9.3.1 Utathmini wa dalili za kliniki ya hali iliyozuiliwa

Kuna uwezekano zaidi ya leba iliyozuiliwa kutokea iwapo taarifa hizi ni za kweli:

  • Leba ikiwa ni ya muda mrefu (kukaa zaidi ya saa 12).
  • Mama anaonekana kuwa amechoka, anawasiwasi, na amedhoofika.
  • Membreni ya fetasi imepasuka na amnii kutoka saa kadhaa kabla ya leba kuanza.
  • Mama ana dalili muhimu zisizo za kawaida: mpigo wa mshipa wa damu ulio wa kasi, zaidi ya mipigo 100 kwa dakika; kiwango cha chini cha shinikizo la damu; kiwango cha kupumua zaidi ya 30 kwa dakika; pengine kiwango cha joto mwilini kilicho juu.

Tathmini mwanamke aliye na historia hii ya leba kwa kupima uke wake. Yoyote kati ya dalili hizi inaonyesha kuwa kuna leba iliyozuiliwa:

  • Mekoniamu iliyo na harufu mbaya inayotoka ukeni.
  • Mkojo uliomumunyika, ambayo unaweza kuwa na mekoniamu au damu.
  • Edema ya valva, hasa ikiwa mwanamke amekuwa akisukuma kwa muda mrefu. Unahisi uke kuwa moto na kavu kwa kidole chako kilicho na glavu kwa sababu ya upungufu wa maji mwilini. (Edema ni uvimbe kwa sababu ya mkusanyiko wa viowevu wa tishu. Valva ni sehemu siri ya nje ya mwanamke, ikiwa ni pamoja na midomo.)
  • Edema ya seviksi.
  • Unaweza kuhisi uvimbe mkubwa juu ya fuvu ya fetasi (Kaputii, Kipindi cha 4).
  • Kitangulizi au mlalo usiokuwa wa kawaida wa fetasi.
  • Uambatanano duni wa seviksi na kitangulizi (angalia nyuma katika Mchoro 1.1 katika Kipindi cha kwanza somo); kama matokeo seviksi inahisi kama “mkono tupu wa vazi”.
  • Bandl’s ring (Mchoro 9.2).

9.3 Dalili za leba iliyozuiliwa

9.3.2 Bandl’s ring