11.6 Orodha ya ithibati za rufaa ya dharura
Tunakaribia mwisho wa Moduli hii katika Leba na Utunzaji wakati wa Kuzaa. Jedwali 11.1 linatoa kwa muhtasari baadhi ya mambo muhimu ya kukumbuka wakati wa rufaa ya dharura wakati mwanamke anapovuja damu nyingi baada ya kuzaa. Habari hii inasaidia katika hali nyinginezo za dharura zinazotishia maisha kama zilivyoelezwa katika vipindi vya hapo awali. Katika moduli inayofuatia, uendeleshaji wa utunzaji huendelea hadi Utunzaji wa baada ya Kuzaa.
Azimia kudumisha mambo haya: | Hatua |
---|---|
Mkazo wa uterasi | Papasa uterasi taratibu, au uisukume kwa mikono miwili na uendelee kuisukuma hivyo wakati wa rufaa. |
Kibofu kitupu | Ikiwa mwanamke hawezi kukojoa, ingiza katheta inayojishikilia ili kutoa mkojo na uiache ndani ya kibofu wakati wa rufaa. |
Kiasi kinachotosha cha damu | Ikiwa mwanamke anavuja damu au ana mshtuko, mpe viowevu vya mishipa ya vena na uendelee kupima viowevu hivi wakati wa rufaa. |
Dalili muhimu | Chunguza rangi, mrindimo wa damu, shinikizo la damu, halijoto, kupoteza damu na kiwango cha kujifahamu. |
Joto | Mfunike mwanamke huyu kwa blanketi. |
Nafasi | Mwanamke huyu anafaa kulala bapa, huku miguu yake ikiinuka juu ya kipeo cha kichwa chake ili kumsaidia kudumisha shinikizo lake la damu. |
Ujasiri | Mpe mwanamke huyu usaidizi wa kihisia na uhakikisho. Mtulize iwezekanavyo. |
Nakala sahihi na maagizo ya rufaa | Orodhesha matokeo yako yote na hatua za dharura ulizochukua katika maagizo ya rufaa. Jumuisha pia historia ya mwanamke huyu na habari za kina kuhusu utambulisho wake. |
Ni vidokezo vipi viwili muhimu zaidi vya kukumbuka kuhusu kuvuja damu baada ya kuzaa?
Kumbuka vidokezo hivi viwili:
- Ingawa vipengele vya hatari huhusishwa na kuvuja damu baada ya kuzaa, theluthi mbili ya wanawake wanaokumbwa na hali hii hawana vipengele vya hatari vinavyojulikana. Haiwezekani kutabiri ni wanawake wepi watakaokumbwa na hali hii ya kuvuja damu baada ya kuzaa.
- Fahamu kuwa mwanamke yeyote yule anaweza kukumbwa na hali hii akiwa chini ya utunzajii wako anapozaa. Hali hii ni hatari kwa maisha, hivyo unafaa kujiandaa kuchukua hatua inayofaa ya dharura. Hatua hii ni pamoja na kumpa rufaa ya haraka hadi katika kituo cha afya.
Mwisho wa jibu
11.5.3 Udhibiti wa dharura wa kuvuja damu baada ya kuzaa kunakohusiana na jeraha