20. Utokaji mimba na Visababishi vingine vya Kuvuja damu mapema katika Ujauzito

Kipindi cha utokaji mimba na Visababishi vingine vya Kuvuja damu mapema katika Ujauzito

Utangulizi

Katika kipindi hiki utajifunza kuhusu visababishi vikuu vya kuvuja damu mapema katika ujauzito, yaani mwanamke anapovuja damu akiwa mjamzito na kabla ya wiki 28, na halipaswi kutendeka. Kutoka kwa mimba ni mojawapo ya visababishi vya kawaida sana vya kuvuja damu mapema katika ujauzito na ni sababisho kuu la vifo vya kina mama na maradhi yanayohusiana na kuzaa ulimwenguni. Aidha, kati ya mimba 100, 15 hutoka pekee yao (uharibikaji wa mimba). Utajifunza jinsi ya kuainisha utokaji wa mimba ili kutoa utunzaji unaofaa, na mtazamo wa kisheria kuhusiana na utoaji wa mimba na njia salama za kutoa mimba zinazotumika katika vituo vya afya. Mimba isiyo kuwa ya kawaida na katika sehemu yake ni visababishi vingine vikuu vya kuvuja damu mapema katika ujauzito. Mwanamke anaweza kuwa na matatizo ya kiafya akimaliza ujauzito mapema, kwa hivyo unapaswa kujua ishara za onyo. Kipindi hiki kinamalizia na jukumu la kumshauri kuhusu utunzaji wa dharura na rufaa ya awali ambayo inaweza kuokoa maisha ya mwanamke, na ushauri baada ya kutoa mimba na upangaji uzazi.

Malengo ya Somo la Kipindi cha 20