5. Utungisho, Upandikizaji na Kuzunguka kwa Damu kwenye Fetasi na Plasenta
Kipindi cha 5 Utungisho, Upandikizaji, na Mzunguko wa Damu kwenye Fetasi na Plasenta
Utangulizi
Wakati kamili ambapo ova iliyotungishwa, embrio, fetasi, au mtoto mchanga huitwa binadamu ni jambo ambalo limekumbwa na utata. Jambo hili ni tofauti miongoni mwa watu binafsi, vikundi vya kidini, mifumo ya haki, na hata mataifa. Kipindi hiki hakizungumzii wazo hili gumu, bali kinazingatia kuhusu jinsi ova inavyotungishwa na kupandikizwa kwenye uterasi, na jinsi fetasi inavyolishwa wakati wa ujauzito. Kipindi hiki kitakusaidia kutambua vipengele vinavyoweza kupelekea matatizo wakati wa ujauzito.