4. Udhibiti wa Homoni katika Mfumo wa Uzazi wa Kike

Kipindi cha 4 Udhibiti wa Homoni katika Mfumo wa Uzazi wa Kike

Utangulizi

Katika Kipindi kilichopita ulijifunza kuhusu anatomia na fiziolojia ya mfumo wa uzazi wa kike. Homoni za estrojeni na projesteroni ziliangaziwa kwa kifupi. Katika Kipindi hiki, utajifunza mengi zaidi kuhusu wajibu wa homoni hizi na zingine muhimu zinazohusika katika udhibiti wa mzunguko wa hedhi kwa binadamu, utoaji wa ova (mayai) na wanawake wa umri wa uzazi na uandaaji wa uterasi kwa kufaa kuupokea ujauzito.

Malengo ya Somo la Kipindi cha 4