17. Kupasuka kwa Tando kabla ya Wakati (KTW)
Kipindi cha 17 Kupasuka kwa Tando kabla ya Wakati (KTW)
Utangulizi
Katika Kipindi hiki utajifunza kuhusu ufafanuzi, uainishaji na hatari za KTW.Tutaeleza matatizo yanayoweza kusababisha ugonjwa na hata kifo kwa mama.
Kipindi hiki pia kinakujulisha kuhusu matatizo yanayoweza kuhatarisha maisha ya fetasi na mtoto mchanga. Utajifunza jinsi ya kutambua dalili za KTW na hatua ambazo unaweza kuchukua unapokuwa na wanawake walio na shida ya KTW, ukizingatia unayoyajua kuhusu kutokwa na kiowevu kutoka ukeni kama mojawapo ya dalili hatari katika Kipindi cha 15.