1.1.1 Vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na matatizo

Kifo cha mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa hufafanuliwa kama kifo cha mwanamke akiwa mjamzito au katika muda wa siku 42 baada ya mwisho wa ujauzito, bila kuzingatia muda na mahali pa ujauzito, kutokana na visababishi vyovyote vinavyohusiana au kukuzwa na ujauzito au utunzaji wake, bali si kutokana na ajali au visababishi vinavyoambatana na matukio (yaani visababishi vya vifo visivyohusiana na ujauzito huo).

Visababishi vitano vikuu vya vifo vya kina mama kabla,katika na muda mfupi baada ya kuzaa ni:

  • Utoaji mimba usio salama
  • Eklampsia isababishwayo na shinikizo la damu hatari wakati wa ujauzito
  • Vizuizi wakati wa kuzaa
  • Kuvuja damu baada ya kuzaa
  • Maambukizi baada ya kuzaa

Utajifunza kuhusu kila aina ya visababishi hivi kwa kina katika vipindi vya baadaye katika moduli hii. Hapa tunaangazia jinsi data kuhusu vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa hukusanywa na kuripotiwa ili uweze kukadiria vifo hivi katika eneo lako.

Kila mwaka, Shirika la Afya Duniani hukadiria kuwa wanawake 536,000 ulimwenguni hufa kutokana na matatizo ya ujauzito na kuzaa na kuwa asilimia 99 yao wako katika nchi zinazoendelea. Angalau wanawake milioni 7 wanaoongoka katika kuzaa huathiriwa na matatizo mabaya ya kiafya kwa muda mrefu. Pia, wanawake milioni 50 zaidi huathirika kutokana na matokeo mabaya ya kiafya baada ya kuzaa. Mengi ya matatizo haya hutokea katika nchi zinazoendelea (Ripoti ya Shirika la Afya Duniani kuhusu Maendeleo ya kutimiza Malengo ya Milenia ya Maendeleo iliyochapishwa mwaka 2009).

Kila mwaka barani Afrika, wanawake milioni 30 hushika mimba na milioni 18 kati yao huzalia nyumbani bila kuhudumiwa na mtaalamu wa afya mwenye ujuzi. Kutokana na haya, wanawake waafrika zaidi ya 250,000 hufariki kila mwaka kutokana na matatizo yanayohusiana na ujauzito na kuzaa. Wanawake waafrika milioni 4 wana matatizo ya ujauzito yasiyo hatari (Okoa Watoto, USAID, UNFPA, UNICEF, WHO, Nafasi kwa Watoto Wachanga Waafrika; Data tendaji, Hati na utaratibu mwafaka wa kusaidia utunzaji wa watoto wachanga Afrika, mwaka 2006).

  • Ni sehemu gani ya vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa duniani hutokea barani Afrika?

  • Wanawake Waafrika wanachangia karibu nusu ya wanawake 536,000 wanaofariki kila mwaka duniani kutokana na matatizo ya ujauzito au kuzaa.

    Mwisho wa jibu

Uwiano wa Vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa

Njia bora zaidi ya kulinganisha viwango vya vifo vya kina mama vitokanavyo na ujauzito katika maeneo tofauti ya dunia ni kukokotoa uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa ambao hukuonyesha idadi ya vifo vya kina mama kwa kila watoto 100,000 wazaliwao wakiwa hai. Uwiano huu umetambuliwa kimataifa kama mojawapo ya viashirio muhimu vya afya ya kina mama na ubora wa utunzaji katika ujauzito, kuzaa na baada ya kuzaa katika nchi fulani. Baadaye katika kipindi hiki, tutakuonyesha jinsi ya kukokotoa uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa katika eneo lako.

Ukaguzi wa demografia na Afya uliofanywa mwaka wa 2000 na 2005 umeonyeshamakadirio ya uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa katika nchini humo. Mwaka wa 2000, kina mama 871 walifariki kutokana na matatizo ya ujauzito au kuzaa kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai barani Afrika. Kufikia mwaka wa 2005, idadi hii ilikuwa imepungua hadi 673 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai. Hii ni chini ya 900 kwa kila watoto 100,000 wazaliwao wakiwa hai katika Afrika nzima. Hii bado ni mojawapo ya viwango vya juu sana duniani. Katika mwaka 2008, wastani wa dunia nzima wa uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa ulikuwa vifo 400 vya kina mama kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai. Wastani wa Uropa ulikuwa 27 tu kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai.

Mchoro 1.1 Sehemu ya uzazi uliofanyika Nyumbani na Hospitalini katika mwaka wa 2005.

Barani Afrika mwaka wa 2005, takribani wanawake milioni 3,119,000 walizaa. Mchoro 1.1 unaonyesha kuwa asilimia 94 ya uzazi huu ulifanyika nyumbani - hasa katika jamii za vijijini kama yako (Ukaguzi wa demografia na Afya uliofanywa Barani Afrika mwaka wa 2005).

  • Kokotoa idadi ya vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa barani Afrika mwaka wa 2005 ukizingatia uwiano wa vifo vya kina mama kwa mwaka huo.

  • Uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa katika mwaka wa 2005 ni 673 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai na kulikuwa na wachanga 3,119,000 kwa jumla mwaka huo. 3,119,000 ikigawanywa na 100,000 ni 31.19. Kwa hivyo, nchini humo kwa jumla, 31.19 x 673 ni wanawake 20,991 waliofariki kutokana na matatizo ya ujauzito au kuzaa.

    Mwisho wa jibu

Ingawa uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa huwapa wanaotengeneza sera za afya ya umma kipimo cha ukubwa wa tatizo la vifo hivi vya kina mama, hauwezi kutufahamisha kuhusu utatuzi unaohitajika kwa kuokoa maisha ya wanawake. Kusoma katika moduli hii yenye mchanganyiko wa mafunzo na mbili zifuatazo, ambazo zinahusu utunzaji katika leba, katika kuzaa na baada ya kuzaa pamoja na mafunzo tendaji husika kwa moduli hizi kutakuwezesha kupunguza vifo vya kina mama katika jamii yako.

1.1 Vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na vya watoto wachanga

1.1.2 Vifo vya watoto wachanga na matatizo