1.2 Kupangia mama mjamzito na mtoto mchanga utunzaji wa kiafya katika jamii yako

Wanawake wajawazito wanaweza kukabiliwa na matatizo mengi tofauti ya kiafya katika ujauzito. Baadhi ya haya ni kutokwa na damu, shinikizo la juu la damu mwilini, mitukutiko, kiwango cha juu cha joto, kiwaa, maumivu ya fumbatio, ugumu wa kupumua, maumivu makali ya kichwa, anemia, kisukari na maambukizi mengine. Utajifunza juu ya utambuzi na jinsi ya kudhibiti matatizo haya yote ya kiafya katika masomo ya baadaye ya moduli hii.

Ili kuhakikisha ufahamu kamili wa matatizo ambayo wanawake wajawazito wanaweza kukabiliwa nayo katika kipindi cha ujauzito na utatuzi unaoweza kutumika, mpango maalumu wa utunzaji unaofaa kabla ya kuzaa ni muhimu. Msingi wa maudhui ya mpango huo na utaratibu wa mtazamo unapaswa kuwa uwasilishaji wa jumbe wazi za kielimu (jinsi utakavyoona katika kipindi cha 2).

Kwa kupanga huduma bora ya afya kwa kina mama wajawazito na watoto wachanga, unahitaji kufanya makadirio ya jamii yako na kutambua mahitaji ya kiafya ya watu.

  • Unawezaje kufanya haya?

  • Unaweza kufanya makadirio haya kwa kuuliza maswali au kupitia majadiliano na waakilishi wa jamii na wazee wanaojua mwelekeo unaodumu wa tabia, mila, mitazamo na maadili katika jamii, ambayo hupokezwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

    Mwisho wa jibu

Kisha unahitaji kutambua matatizo kwa mujibu wa hali ya kiafya ya kina mama wajawazito na watoto wachanga na kutathmini matumizi ya huduma. Katika kuendeleza huduma za afya kwa kina mama wajawazito na watoto, unapaswa kutambua wazi mitazamo na hali zozote zilizo na athari kwa matokeo. Kwa mfano, katika vijiji vidogo, mwanamke anapokuwa na tatizo wakati wa kuzaa ni vigumu sana kwenda katika kituo cha afya au hospitali. Ni wanakijiji wachache sana walio na magari, na hata mijini, madereva wengi wa teksi hukataa kumpeleka hospitalini mwanamke aliye katika uchungu wa kuzaa. Kwa hivyo ni muhimu sana kuwa na mpango wa huduma ya dharura, na kuwa na mipango ya kuwasafirisha wanawake wanaohitaji huduma za haraka za kutibu matatizo yanayohusiana na ujauzito au kuzaa. Utajifunza kuhusu mipango ya huduma za dharura katika kipindi cha 13.

Kuchunguza kinachowatatiza watu katika jamii yako ni hatua muhimu ya kwanza katika kutambua na kutafiti matatizo katika eneo lako. Hatua ifuatayo ni kuyapanga katika utaratibu wa kipaumbele.

1.1.3 Je, vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na vya watoto wachanga vinawezaje kupunguzwa?

1.2.1 Kupanga matatizo ya kushughulikia kwa msingi wa kipaumbele