1.2.1 Kupanga matatizo ya kushughulikia kwa msingi wa kipaumbele

Unapaswa kuyapanga matatizo yaliyoainishwa kwa msingi wa vigezo vifuatavyo:

  • Ukubwa wa tatizo (Je,tatizo hili ni kubwa kiasi gani?)
  • Uzito wa tatizo (Je, tatizo hili lina uzito upi kulingana na matokeo mabaya?)
  • Uwezekano wa kutatua (Je, ni njia ipi iliyo rahisi au ngumu kwa kukabiliana na tatizo hili?)
  • Tatizo kwa jamii (Je, tatizo hili lina umuhimu upi kwa jamii?)
  • Tatizo kwa serikali (Je, lina umuhimu upi kwa serikali?).

Kwa mfano, ikiwa kuna upungufu wa huduma kwa kina mama wajawazito na uchache wa vyoo katika eneo lako, unaweza kupanga kwa msingi wa kipaumbele matatizo haya mawili, kama inavyoonyeshwa katika Jedwali 1.1. Mfumo wa kutuza alama ni 1- 5, ambapo 1 ni ya chini zaidi na 5 ni ya juu zaidi. Unaamua juu ya tuzo katika kila sanduku katika jedwali kwa kuzingatia ufahamu wako wa jamii yako na mahitaji yake.

Jedwali 1.1 Mfano wa uchambuzi wa matatizo mawili yaliyotambuliwa kulingana na kipaumbele
Tatizo lililotambuliwaUkubwaUkubwa wa tatizoUwezekanoKinachotatiza jamiiKinachotatiza serikaliIdadi kamili kwa (kwa 25)
Upungufu wa kiwango cha hudumu za kabla ya kuzaa 5555525
Upungufu wa matumizi ya vyoo5444421

Unavyoona katika Jedwali 1.1, alama ya jumla ni 25 kwa upungufu wa kiwango cha huduma zifaazo katika ujauzito na 21 kwa upungufu wa matumizi ya vyoo. Kwa hivyo, katika mfano huu, ungeweka upungufu wa kiwango cha huduma kwa kina mama katika ujauzito kama tatizo litakalopewa kipaumbele. Baada ya kutambua tatizo litakalopewa kipaumbele katika jamii yako, hatua zifuatazo zimeorodheshwa katika kisanduku 1.1.

Kisanduku 1.1 Hatua katika kushughulikia tatizo.

  • Weka malengo (k.m kuongeza idadi ya wanawake wanaopata huduma ya utunzaji kabla ya kuzaa)
  • Tambua mikakati utakayotumia kufanikisha haya (k.m kwa kuandaa kampeni ya elimu ya kiafya ili kuendeleza faida za huduma ya kabla ya kuzaa - kama ilivyoelezwa katika somo la 2)
  • Tambua rasilimali zinazohitajika kwa utekelezaji wa mpango wako
  • Weka kipindi maalumu cha muda wa kutimiza malengo yako
  • Endelea kufuatilia na kutathmini jinsi unavyoendelea katika kutimiza malengo yako.

1.2 Kupangia mama mjamzito na mtoto mchanga utunzaji wa kiafya katika jamii yako

1.2.2 Kukokotoa idadi ya wanawake wanaohitaji huduma za kabla ya kuzaa