1.2.2 Kukokotoa idadi ya wanawake wanaohitaji huduma za kabla ya kuzaa

Hatua ya kwanza katika kutathmini haja ya huduma ya utunzaji katika ujauzito katika jamii yako ni kukokotoa idadi ya wanawake wanaoweza kushika mimba katika mwaka wa kawaida. Wakati mwingine wanawake hawa hujulikana kama wanaostahili utunzaji wa kabla ya kuzaa.

Wasifu wa jamii hueleza ukubwa na sifa bainifu za jamii na vipengele vikuu vya afya vinavyowaathiri watu. Takwimu za watu pamoja na ukweli na tarakimu juu ya afya ya kina mama wajawazito na ujauzito katika jamii na habari kuhusu jinsi shughuli za kijamii zinavyotekelezwa ni habari muhimu kwa kupanga na kuendeleza utunzaji kabla ya kuzaa. Lakini kumbuka kwamba kila jamii ni tofauti. Kwa hivyo, mifano tunayotoa katika sehemu hii inaweza kutofautiana na utakayopata katika jamii yako.

Kulingana na takwimu za watu barani Afrika, idadi ya wanawake wajawazito hukokotolewa kama asilimia 4 ya watu kwa jumla. Asilimia hii itabadilika kwa kiasi fulani kati ya jamii kulingana na idadi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa miongoni mwa watu. Idadi ya wanawake wanaostahili utunzaji kabla ya kuzaa katika mwaka mmoja barani Afrika inaweza kukadiriwa kwa usahihi wa kutosha kwa kutumia tarakimu ya asilimia 4.

Zoezi 1.1 Kukokotoa idadi ya wanaostahili kupata huduma za utunzaji katika ujauzito katika jamii.

Dhania kuwa idadi kamili ya watu katika jamii moja ni 5,000. Kokotoa idadi ya wanawake wajawazito walio na uwezekano wa kustahili utunzaji katika ujauzito katika jamii hii kwa mwaka mmoja.

Answer

Idadi kamili ya wanawake wajawazito hukokotolewa kama asilimia 4 ya watu 5,000. Ili kukokotoa asilimia 4 ya 5,000, unazidisha 5000 mara 4 kisha ugawanye jawabu na 100. Njia nzuri ya kuandika haya ni kama ifuatavyo:

Kwa hivyo, jamii hii inatarajiwa kuwa na wanawake wajawazito 200 kwa mwaka mmoja wanaostahili utunzaji katika ujauzito, kuzaa na huduma baada ya kuzaa. Ikiwa unajua idadi ya watu katika jamii yako, tumia tarakimu ya asilimia 4 kukokotoa idadi ya wanawake wajawazito watakaohitaji huduma zako katika mwaka mmoja. Andika hesabu yako katika shajara yako ya masomo na umwonyeshe mkufunzi wako katika Kipindi kitakachofuata cha masomo cha kusaidiana.

Mwisho wa jibu

1.2.1 Kupanga matatizo ya kushughulikia kwa msingi wa kipaumbele

1.2.3 Kukokotoa idadi ya vipimo vilivyonuiwa vya utunzaji katika ujauzito