1.2.3 Kukokotoa idadi ya vipimo vilivyonuiwa vya utunzaji katika ujauzito

Wanawake walio na utunzaji katika ujauzito wanaweza kuzaa salama na kuwapata watoto wenye afya njema. Mbinu ifaayo zaidi kwa kutoa huduma kwa wajawazito imebuniwa katika miaka ya karibuni. Mbinu hii mpya huitwa utunzaji ulionuiwa wa kabla ya kuzaa. Ni ratiba ya awamu nne iliyopendekezwa kwa mwanamke mjamzito asiye na matatizo makubwa ya kiafya. Ratiba ya awamu hizi nne zilizonuiwa ni kama ifuatavyo:

Ziara Muda
Awamu ya kwanzaZaidi ya wiki 16 ya ujauzito
Awamu ya piliKati ya wiki 24 na 28
Awamu ya tatu Kati ya wiki 30 na 32
Awamu ya nneKati ya wiki 36 na 40

Utajifunza cha kufanya kwa undani katika kila kipimo kilichonuiwa kwa utunzaji katika ujauzito katika kipindi cha 13.

  • Tazama jibu la zoezi 1.1. Ni awamu ngapi za utunzaji katika ujauzito utakazokuwa nazo katika jamii hiyo kwa mwaka mmoja ikiwa ulitimiza utunzaji ulionuiwa kwa kila mwanamke mjamzito?

  • Ungekuwa na awamu 800 za utunzaji katika ujauzito (awamu 4 kwa kila mmoja wa wanawake wajawazito 200)

    Mwisho wa jibu

Jawabu hili hueleza jinsi utakavyohitaji kupanga huduma zako za ujauzitoni kwa umaakini, ikiwa utamtembelea kila mwanamke mjamzito mara nne! Kama huwezi kutimiza idadi hii, unapaswa kutembelea kila mwanamke mjamzito angalau mara moja, na unakili awamu kama ilivyoelezwa katika sehemu inayofuata.

1.2.2 Kukokotoa idadi ya wanawake wanaohitaji huduma za kabla ya kuzaa

1.2.4 Kukokotoa kiwango cha utumiaji wa huduma zifaazo katika ujauzito