1.2.5 Kukokotoa sehemu ya wanawake waliozaa kwa kuhudumiwa na` wataalamu wa afya

Vilevile, kufanikiwa katika kupanga huduma za kuzaa kunaweza kutathminiwa kwa kukokotoa asilimia ya wanawake wanaojifungua kwa kuhudumiwa na mtaalamu wa afya na kugawanywa na idadi kamili ya wanaotarajiwa kuzaa katika kipindi cha muda fulani (kwa kawaida mwaka mmoja) katika eneo hilo (mara 100).

Kulingana na ukaguzi wa demografia na Afya uliofanywa barani Afrika mwaka wa 2005, waliozaa kwa kuhudumiwa na mhudumu wa uzazi mwenye ujuzi ni asilimia 6 tu. Mhudumu huyu ni mtu ambaye huwa amepata mafunzo ya ujuzi wa ukunga kufikia kiwango cha ustadi muhimu wa kusimamia wanaozaa kwa kawaida na kuweza kutambua, kudhibiti au kupendekeza rufaa kwa matibabu mbadala kukiwa na matatizo ya ukunga. Ni lazima awe na uwezo wa kutambua mwanzo wa matatizo, kuingilia kati kwa kufanya shughuli fulani muhimu, kuanza matibabu, na kusimamia rufaa kwa matibabu mbadala ya mama na mtoto matatizo yakizidi uwezo wao au yakiwa hayawezekani katika mazingira hayo. Afrika ina kiwango cha chini zaidi duniani cha wanaozaa kwa kuhudumiwa na wenye ujuzi wa uzazi. Kukokotoa asilimia ya wanaojifungua kwa kuhudumiwa na mhudumu wa uzazi mwenye ujuzi ni ifuatavyo:

  • Kokotoa kiwango cha wanaozaa kwa kuhudumiwa na wahudumu wenye ujuzi ikiwa ulihudumia wanawake 150 kati ya 200 waliozaa katika eneo lako.

  • Itakuwa

    150/200 x 100 = 75%

    Mwisho wa jibu

Kutimiza kiwango cha juu cha wanaozaa kwa kuhudumiwa kutakusaidia kupunguza vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na vya watoto wachanga na matatizo katika jamii yako. Katika sehemu mbili zijazo, tunakuonyesha jinsi ya kukokotoa viwango vya vifo hivi.

1.2.4 Kukokotoa kiwango cha utumiaji wa huduma zifaazo katika ujauzito

1.2.6 Kukokotoa uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa