Muhtasari wa kipindi 1

Katika kipindi hiki,umejifunza kuwa:

  1. Kila mwaka duniani kote, karibu wanawake nusu milioni hufariki kutokana na matatizo ya ujauzito na kuzaa, angalau million 7 hupatwa na matatizo makubwa ya kiafya kwa muda mrefu, na wengine milioni 50 hupatwa na athari mbaya sana. Vingi vya vifo hivi na matatizo hutokea katika nchi zinazoendelea, hasa Afrika.
  2. Ulimwenguni, karibu watoto wachanga millioni 3 hufariki katika majuma 4 ya kwanza baada ya kuzaliwa na pia kuna million 3 wanaozaliwa wakiwa wamefariki. Afrika huchangia asilimia 11 ya idadi ya watu duniani, lakini ina asilimia 25 ya vifo vyote vya watoto wachanga.
  3. Uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa barani Afrika mwaka wa 2005,ulikuwa 673 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai. Kiwango cha vifo vya watoto wachanga katika mwaka huo kilikuwa vifo 39 kwa kila watoto 1,000 waliozaliwa wakiwa hai.
  4. Malengo ya Milenia ya Maendeleo ya Shirika la Afya Duniani yaliyowekwa mwaka wa 2000 yana makusudio yaliyowekwa kwa kupunguza vifo vya watoto kwa thuluthi mbili na vifo vya kina mama wajawazito kwa robo tatu kufikia mwaka wa 2015.
  5. Upungufu mkubwa unaweza kutimizwa kupitia uhamasishaji mwafaka wa jamii, elimu ya kiafya, huduma za kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa zilizopangwa vizuri na uthibiti kamilifu wa maradhi ya watoto wachanga na ya utotoni.
  6. Ukadiriaji wa jamii yako na utambuzi wa mahitaji ya watu ya kiafya unaweza kufanywa kwa kuuliza maswali au majadiliano na wawakilishi wa jamii na wazee.
  7. Unaweza kukadiria idadi ya wanawake ambao wanastahili kupata huduma za kabla ya kuzaa kwa mwaka mmoja katika eneo lako ukiwa na usahihi wa kutosha kwa kukokotoa asilimia 4 ya watu wote kwa jumla katika eneo hilo.
  8. Unaweza kukokotoa kiwango cha wanaopata huduma za kabla ya kuzaa kutoka kwa idadi kamili ya kina mama wajawazito uliohudumia angalau mara moja kwa ajili ya sababu zinazohusiana na ujauzito wao na kugawanya na idadi kamili ya wanawake wajawazito wanaotarajiwa katika eneo lako kwa mwaka mmoja (× 100%).
  9. Unaweza kukadiria kiwango cha kuzaa kwa kupata huduma kwa kukokotoa uwiano wa uliohudumia wakizaa na kugawanya na idadi kamili ya wanaotarajiwa kuzaa katika mwaka mmoja (× 100%).
  10. Njia moja ya kukadiria ufaafu wa huduma zako za kabla na wakati wa kuzaa ni kukokotoa uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa wakiwa hai na kiwango cha vifo vya watoto wachanga kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai katika eneo lako ili kujua kama vinapungua kila mwaka.

1.2.7. Kukokotoa kiwango cha vifo vya watoto wachanga

Maswali ya kujitathmini kwa kipiondi cha 1