4.1 Homoni za uzazi wa kike

Jinsi unavyoweza kukumbuka kutoka katika somo lako la biolojia katika shule ya upili hapo awali, majukumu mbalimbali ya mwili hudhibitiwa na mfumo wa neva na wa homoni. Mifumo hii miwili huhusika katika udhibiti wa shughuli za mfumo wa uzazi wa kike kwa mfuatano wa matukio ya kila mwezi yaitwayo mzunguko wa hedhi, jinsi tutakavyoelezea.

Unapaswa kukumbuka kutoka katika Kipindi cha 3 kwamba homoni ni kemikali ya kutuma ishara ambayo hutengenezwa mwilini na kuenea katika damu. Homoni tofauti hudhibiti shughuli za seli au ogani tofauti. Majukumu ya homoni tano kuu zinazodhibiti mfumo wa uzazi wa kike yameelezewa katika Kisanduku 4.1 na kisha jinsi zinavyoingiliana kuelezewa katika mchoro 4.1.

Kisanduku 4.1 Homoni zinazodhibiti mfumo wa uzazi wa kike

Homoni itoayo gonadotropini hutolewa na sehemu ya ubongo iitwayo hipothalamasi. Homoni hii ieneapo katika damu husababisha kutolewa kwa homoni mbili muhimu (tazama hapa chini na pia mchoro 4.1) kutoka kwa tezi ya pituitari iliyo katika sehemu nyingine maalumu ya ubongo.

Homoni Chochelezi ya Foliko (HCF) hutolewa na tezi ya pituitari katika nusu ya kwanza ya mzunguko wa hedhi. Homoni hii huchochea ukuaji wa foliko pevu ya ovari na kudhibiti utoaji wa ova na manii kwa mwanamke na mwanamume mtawalia.

Homoni ya lutea pia hutolewa na tezi ya pituitari iliyo ubongoni. Homoni hii huchochea ovari kutoa estrojeni na projesteroni. Pia huchokonoa ovulesheni (kutolewa kwa ova pevu kutoka kwenye ovari) na kuendeleza kukua kwa kopasi luteamu.

  • Je, kopasi luteamu ni nini? (Kumbuka Kipindi cha 3)

  • Jina kopasi luteamu humaanisha ‘mwili wa manjano,’na hukua katika ovari baada ya ovulesheni kutoka kwa foliko za ovari zilizokua na kutoa ova.

    Mwisho wa jibu

    Estrojeni ni homoni ya uzazi wa kike ambayo hutolewa hasa na ovari kwa mwanamke asiye na ujauzito. Homoni hii huendeleza upevukaji na utolewaji wa ova katika kila mzunguko wa hedhi. Pia hutolewa na kondo wakati wa ujauzito.

    Projesteroni hutolewa na kopasi leteamu katika ovari. Jukumu la homoni hii ni kuandaa endometriamu (bitana ya uterasi) kwa kupokea na kukuza ova iliyotungishwa. Pia hukomesha utoaji wa estrojeni baada ya ovulesheni.

Mchoro 4.1 Udhibiti wa homoni katika mfumo wa uzazi wa kike.

Muda wa mzunguko wa hedhi huwa ni takribani siku 28 lakini unaweza kuwa wa kubadilika. Muda huu unaweza kuwa mfupi kama wa siku 21 au mrefu kama wa siku 39 kwa wanawake wengine. Mzunguko huu wa hedhi hueleweka vizuri tukilenga kwanza shughuli zinazotendeka katika ovari kisha zinazotendeka katika uterasi. Tutaeleza kila moja ya hizi.

Malengo ya Somo la Kipindi cha 4

4.2 Mzunguko katika ovari