4.4 Kuvunja ungo, kubaleghe na ukomohedhi

Huenda unajua kuwa kuvunja ungo (hedhi ya kwanza), kwa wastani, huanza kati ya umri wa miaka 12 hadi 15 katika bara la Afrika. Hata hivyo, katika hali zingine huenda ianze baadaye kwa kuchelewa kati ya umri wa miaka 17 hadi 20 au mapema kati ya umri wa miaka 8 hadi 9. Baadhi ya mambo yanayoathiri umri wa kuvunja ungo ni ya kibayolojia na mengine ni ya kitamaduni.

Kuvunja ungo (hedhi ya kwanza) huanza hipothalamasi kwenye ubongo inapochochewa kuanza kutoa homoni itoayo gonadotropini katika umri wa takribani miaka 12 hadi 15. Hata hivyo, imethibitishwa kuwa homoni itoayo gonadotropini inaweza kuanza kutolewa kwa umri wa chini kwa wasichana waliostawishwa vyema na kutangamana na mambo yanayozidisha hamu ya ngono kama vile kutazama filamu za ngono na kuongea kuhusu ngono. Huenda hedhi ya kwanza (kuvunja ungo) ichelewe hadi umri wa miaka 17 hadi 20 kwa wasichana wasiostawishwa vyema, na wasiotangamana sana na mambo yanayozidisha hamu ya ngono. Magonjwa yanayoathiri hipothalamasi na tezi ya pituitari au ovari na uterasi yanaweza pia kuathiri umri wa hedhi ya kwanza.

Katika umri wa kuvunja ungo, homoni za uzazi wa kike, estrojeni na projesteroni huwajibika katika kukuza sifa za baadaye za kijinsia kwa mwanamke. Hizi ni:

  • Ukuaji wa matiti
  • Upanukaji wa pelvisi
  • Kuongezeka kwa shughuli za tezi za jasho na za mafuta
  • Uotaji wa nywele za kinena na za kwapani.

Pamoja na hedhi ya kwanza, kujitokeza kwa sifa za baadaye za kijinsia hudhihirisha kipindi kiitwacho ubaleghe – kipindi cha maisha (hasa kati ya umri wa miaka 10 hadi 15) ambapo viungo vya uzazi hukua kikamilifu na kuweza kutenda majukumu yao. Sifa za baadaye za kijinsia huitwa ‘za baadaye’ kwa sababu hutokea baada ya sifa za mwanzo za kijinsia zinazowatofautisha wanawake na wanaume.

  • Taja baadhi ya sifa za mwanzo za kijinsia za wanawake.

  • Tayari ulisoma kuzihusu katika Kipindi cha 3 cha somo -ndivyo viungo vya nje vya jenitalia ya kike (kwa mfano labia ndogo na kisimi), na viungo vya ndani vya uzazi wa kike (kwa mfano ovari,uterasi na uke).

    Mwisho wa jibu

Hedhi huendelea kutoka kila mwezi isipokuwa wakati wa ujauzito hadi mwanamke huyo atakapofikia ukomohedhi kati ya takribani umri wa miaka 48 hadi 50 ambapo hedhi hukoma. Unaweza kukumbuka kutoka katika Kipindi cha somo cha 3 kuwa wakati wa kuzaliwa, ovari za mtoto mchanga wa kike anapozaliwa tayari huwa na takribani ova 60,000 zisizopevu na hawezi kutoa zingine zaidi maishani mwake. Anapofikia ukomohedhi, uwezo wake wa kupevusha ova hufika mwisho.

Tutaelezea katika Kipindi cha 5 cha somo kinachotendeka ova inapotungishwa na kujipandikiza kwenye uterasi na kukua hadi itakapokuwa fetasi.

4.3.3 Awamu ya unyesaji: siku ya 15 hadi ya 28

Muhtasari wa Kipindi cha 4