Muhtasari wa Kipindi cha 4

Umejifunza katika Kipindi cha 4 cha somo kuwa:

  1. Homoni zinazoudhibiti mfumo wa uzazi wa kike ni homoni itoayo gonadotropini , homoni chochelezi ya foliko na homoni ya lutea ambazo hutolewa kwenye ubongo; estrojeni na projesteroni zinazotolewa na ovari na kopasi luteamu; na homoni ya binadamu ya korioni ya gonadotropini ambayo hutolewa na plasenta wakati wa ujauzito.
  2. Mzunguko wa hedhi kwa kawaida huchukua siku 28 lakini unaweza kuwa wa kubadilika sana. Hii huonyeshwa na hedhi kutoka siku ya 1 hadi ya 5 na ovulesheni karibu siku ya 14 lakini ni vigumu kutabiri siku ya ovulesheni kwa usahihi.
  3. Hedhi ni kukwangulika kwa kila mwezi kwa endometriamu kutoka kwa uterasi na kutokea ukeni pamoja na damu kiasi kwa kawaida kwa muda wa siku tatu hadi tano. Hedhi huendelea kutoka tangu hedhi ya kwanza (kuvunja ungo) hadi ukomohedhi isipokuwa wakati wa ujauzito. Hedhi inaweza pia kukomeshwa na unyonyeshaji.
  4. Mzunguko wa ovari ni matukio ya mara kwa mara yanayojirudia yatendekayo kwenye ovari wakati wa mzunguko wa hedhi. Matukio haya huonyeshwa na ukuaji wa foliko kadhaa za ovari, upevukaji na utoaji (ovulesheni) wa ova moja, na utengenezwaji na kisha usawijikaji wa kopasi luteamu iwapo ujauzito hautatokea.
  5. Mzunguko wa uterasi ni matukio ya mara kwa mara yanayojirudia yatendekayo kwenye uterasi wakati wa mzunguko wa hedhi. Mzunguko huu huonyeshwa na unenepaji wa endometriamu, kuongezeka kwa damu na hatimaye kua nyeusi, kukwangulika na kutolewa kama hedhi iwapo ujauzito hautatokea.
  6. Kuvunja ungo (hedhi ya kwanza) na kujitokeza kwa sifa za baadaye za kijinsia huashiria kipindi cha ubaleghe ambapo ogani za ndani za uzazi hukua kikamilifu na msichana kuwa na uwezo wa kupata ujauzito.

4.4 Kuvunja ungo, kubaleghe na ukomohedhi

Maswali ya kujitathmini ya Kipindi cha 4