Maswali ya kujitathmini ya Kipindi cha 4

Kwa kuwa umekamilisha Kipindi hiki cha somo, unaweza kutathmini ni kwa kiwango kipi umeweza kuyatimiza malengo ya masomo ya Kipindi hiki kwa kujibu maswali haya. Yaandike majibu katika shajaradaftari lako kisha uyajadili na mkufunzi wako katika mkutano utakaofuata wa masomo ya kusaidiana. Unaweza kuyalinganisha majibu yako na Muhtasari juu ya Maswali ya kujitathmini mwishoni mwa Moduli hii.

Swali la kujitathmini 4.1 (linatathmini Malengo ya Somo 4.1 na 4.2)

Safu yakushoto ya Jedwali 4.1 inaonyesha majina ya awamu tofauti zilizo kwenye mzunguko wa hedhi. kamilisha safu ya kushoto kwa kujaza kipindi sahihi tangu kipindi cha mwisho cha kawaida cha hedhi.

Jedwali 4.1 Kwa swali la kujitathmini 4.1
Awamu ya mzunguko wa hedhi Siku (1 = siku ya kwanza ya kipindi cha mwisho cha kawaida cha hedhi)
Awamu ya foliko ya mzunguko katika ovari
Awamu ya lutea ya mzunguko katika ovari
Awamu ya hedhi ya mzunguko katika uterasi
Awamu ya kuongezeka ya mzunguko katika uterasi
Awamu ya unyesaji ya mzunguko katika uterasi

Answer

Jedwali 4.1 Lililokamilishwa.
Awamu ya mzunguko wa hedhi Siku (1 = siku ya kwanza ya kipindi cha mwisho cha kawaida cha hedhi)
Awamu ya foliko ya mzunguko katika ovari1-14
Awamu ya lutea ya mzunguko katika ovari15-28
Awamu ya hedhi ya mzunguko katika uterasi1-5
Awamu ya kuongezeka ya mzunguko katika uterasi6-14
Awamu ya unyesaji ya mzunguko katika uterasi15-28

Swali la kujitathmini 4.2 (linatathmini Malengo ya Somo 4.2)

Je, kwa nini unafikiri kuwa mwanamke anaweza kuhisi maumivu ya mbano kwenye fumbatio lake wakati wa hedhi?

Answer

Mwanamke anaweza kuhisi maumivu ya mbano kwenye fumbatio lake wakati wa hedhi kwa sababu kuta zenye misuli za uterasi (miometriamu) hubana ili kusaidia kukatiza damu iendayo kwenye endometriamu na kuifanya itengane na uterasi.

Mwisho wa jibu

Swali la kujitathmini 4.3 (linatathmini Malengo ya Somo 4.3)

Je, unaweza kupendekeza jinsi viwango vya juu vya estrojeni na projesteroni bandia zipatikanazo kwenye tembe za kuzuia mimba zinavyozuia ujauzito kwa wanawake wanaozitumia tembe hizi mara kwa mara na walivyoshauriwa?

Answer

Kiwango cha juucha estrojeni na projesteroni bandia kwenye tembe za kuzuia mimba huzuia ujauzito kwa kuleta mwitiko hasi kwa utaratibu wa utendaji kazi wa hipothalamasi iliyo kwenye ubongo. Kiwango hiki cha juu cha estrojeni na projesteroni huiga hali inayotokea wakati wa ujauzito. Homoni hizi hukandamiza utoaji wa homoni itoayo gonadotropini kwenye hipothalamasi na kwa hivyo tezi ya pitutari hukoma kutoa homoni chochelezi ya foliko na homoni ya lutea. Hii hatimaye hukomesha ovari kupevusha ova zozote zaidi na kisha mwanamke huyu kamwe hawezi kupata ujauzito almradi anakunywa tembe hizi za kuzuia ujauzito mara kwa mara jinsi alivyoshauriwa.

Mwisho wa jibu

Swali la kujitathmini 4.4 (linatathmini Malengo ya Somo 4.3)

Eleza ni kwa nini hedhi hukoma wakati wa ujauzito.

Answer

Kwa mwanamke mjamzito, kondo huendelea kutoa homoni ya binadamu ya korioni ya gonadotropini inayoichochea kopasi luteamu kwenye ovari kutoa projesteroni katika muda wote wa ujauzito. Projesteroni hudumisha endometriamu kama rusu nene yenye mafuta na kwa hivyo hedhi hukoma wakati wa ujauzito kwa sababu endometriamu bado imejishikiza kwenye uterasi huku ikisaidia katika kustawisha na kuilinda fetasi inayokua.

Mwisho wa jibu.

Muhtasari wa Kipindi cha 4