8.2.2 Dalili na ishara zinazoelekea kuashiria ujauzito
Hizi ni za kutegemewa sana kuliko dalili zinazoweza kutokea lakini si ishara kamili za ujauzito.
Kutanuka kwa fumbatio
Kuna kutanuka kwa fumbatio (tumbo) hatua kwa hatua kutoka juma la 7 hadi la 28 la ujauzito. Katika juma la 16 hadi la 22, ukuaji unaweza kuonekana kuwa wa haraka sana uterasi inapoinuka juu kwenye fumbatio.
Je, unaweza kupendekeza mambo mengine yanayoweza kusababisha utanukaji wa fumbatio?
Dhahiri mno ni kuwa mwanamke huyo ananenepa tu. Lakini pia unapaswa kuwazia ikiwa anaweza kuwa na saratani au aina nyingine ya uvimbe tumboni mwake.
Mwisho wa jibu
Kipimo cha ujauzito cha korioni ya gonadotropini ya binadamu
Homoni hii hutolewa na sehemu ya kiiinitete siku nane tu baada ya utungisho, kisha na plasenta muda wote wa ujauzito. Inaweza kuguduliwa na vipimo vya kemikali ambavyo kwa kawaida vinaweza kufanywa tu katika vituo vya afya vya kiwango cha juu. Vifaa vya kupima ujauzito vinaweza kununuliwa kutoka kwa maduka mengine ya dawa ingawa ni ghali.
Homoni hiyo inaweza kugunduliwa katika damu na mkojo wa mama siku 8 hadi 10 baada ya utungisho au siku 40 baada ya kipindi cha mwisho cha hedhi. Watu wanaposema ‘kipimo cha ujauzito’, wao humaanisha kipimo cha mkojo cha korioni ya gonadotropini ya binadamu. Ingawa hutoa kiashiria bora cha ujauzito kwa watu wengi, vifaa vya kupima vinaweza kutoa matokeo yasiyo ya kweli, hasa ikiwa havikuwa vimehifadhiwa vizuri, au vimepitisha tarehe. Pia kuna magonjwa mengine yasababishayo kutolewa kwa korioni ya gonadotropini ya binadamu.
Minyweo ya uterasi isiyo na maumivu
Uterasi inapotanuka huwa ya mviringo na mara nyingi huzunguka kuelekea upande wa kulia. Minyweo ya uterasi isiyo na maumivu huhisika kama mkazo au shinikizo. Huanza ujauzito ukiwa na umri wa majuma 28 na kuongezeka katika idadi ya marudio. Minyweo hii hupotea kwa kutembea au kufanya mazoezi wakati minyweo ya leba halisi huongezeka kwa udhabiti.
8.2.1 Dalili zinazoweza kuashiria ujauzito