Muhtasari wa Kipindi cha 9
Katika Kipindi cha 9, umejifunza kwamba:
- Kila wakati mama anapotembelea kliniki ya wajawazito, unapaswa kutathmini wajawazito wote kwa ishara na dalili za lishe duni au upungufu wa madini ya iodini, pamoja na weupe, ukosefu wa nguvu na uwepo wa tezi.
- Wanawake wengi huongeza kilo 9-12 wakati wa ujauzito wa kawaida, lakini ongezeko la uzito si kiashiria cha uhakika wa matokeo ya mimba. Ongezeko la uzito kwa ghafla karibu na kipindi cha mwisho wa mimba ni onyo la kuwa kuna uwezekano wa hali prekilampsia na lazima apewe rufaa kwenye kituo cha afya.
- Joto jingi mwilini (joto zaidi ya Nyuzi 37.5) inapaswa kutibiwa mwanzo na viowevu, paracetamol, na kupanguza mwili kwa maji baridi. Mpe mjamzito rufaa kwenye kituo cha afya kama hali yake ya joto itabaki juu. Anahitaji kuchunguzwa kwa magonjwa kama vile malaria.
- Kama kiwango cha mpigo wa mshipa kitaongezeka zaidi ya midundo 100 kwa dakika moja, ni ishara ya ugonjwa na anahitaji rufaa kwenye kituo cha afya.
- Ishara na dalili za anemia ni pamoja na weupe, uchovu, mpigo kwa mshipa wa haraka, na ugumu wa kupumua. Rufaa wajawazito walio na hali hizi.
- Upungufu wa pumzi huwa kawaida karibu na kipindi cha mwisho cha ujauzito vile mtoto anayekuwa hufinya mapafu ya mama. Mpe rufaa iwapo itasababisha usumbufu mkubwa.
- Kama shinikizo la damu ya mama mjamzito itafika mmHg 140/90 au zaidi, ana shinikizo la juu la damu. Kila shinikizo la juu la damu katika ujauzito ni ugonjwa mkali, ambayo inahitaji rufaa mara mojakwa kituo cha afya.
- Mchozo usio wa kawaida kutokea ukeni, kuwashwa au uvimbe wa viungo vya uzazi, na uchungu wakati wa kukojoa au wa ngono, ni dalili za maambukizi kwa uke, na ni lazima apewe rufaa.
Back to previous pagePrevious
9.10 Hitimisho