9.5 Kuchunguza dalili za anemia
Wakati mtu ana anemia, kawaida inamaanisha kwamba hajaweza kula vyakula vilivyo na madini ya ioni ya kutosha. Madini ya ionihusaidia seli za damu nyekundu kubeba oksijeni kutoka kwa hewa tunayovuta hadi kwa sehemu zote za mwili. Baadhi ya aina za anemia husababishwa na ugonjwa, si ukosefu wa ioni. Na baadhi ya aina zingine hurithiwa (maumbile) na haziwezi kutibiwa kwa kula vyakula vyenyeioni au kutumia dawa za ioni. Utajifunza kupima damu, na matibabu ya anemia wakati wa ujauzito, katika Kipindi cha 18, baadaye katika Moduli hii.
Ishara na dalili za afya
Afya njema na nguvu nyingi kwa jumla. Mama hana weupe (angalia sehemu inayofuata).
Ishara na dalili za hatari
- Weupe - weupe ndani ya kope, kucha na ufizi nyeupe (Mchoro 9.7)
- Kizunguzungu au kuzirai
- Udhaifu au kuchoka
- Mpigo kwa mshipa wa mwendo wa kasi (zaidi ya mipigo100 kwa dakika)
- Ugumu wa kupumua (upungufu wa pumzi).
9.4.2 La kufanya iwapo mama ana mipigo kwa mshipa ya haraka