Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 11

Kwa kuwa umekamilisha kipindi hiki, unaweza kutathmini jinsi ulivyotimiza malengo ya masomo haya kwa kujibu maswali haya. Andika majibu katika shajara yako ya masomo na ujadiliane na mkufunzi wako katika Mkutano Saidizi wa Masomo yatakayofuata. Unaweza kulinganisha majibu yako na muhtasari juu ya Maswali ya Kujitathmini mwishoni mwa Moduli hii.

Swali la kujitathmini 11.1 (linatathmini Malengo ya Somo 11.1, 11.2 na 11.3)

Je, ni kauli ipi kati ya hizi isiyo sahihi? Eleza kisicho sahihi katika kila kauli.

  • A.Kusikiza mpigo wa moyo wa fetasi kwa stethoskopu huitwa oskalitesheni.
  • B.Kichwa cha fetasi kikiwa upande wa chini na matako ya fetasi yawe upande wa juu kwenye fandasi, huitwa mlalo wima.
  • C.Katika mlalo wa kutanguliza veteksi, kitanguizi ni matako ya mtoto.
  • D.Kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi huwa takriban mipigo 120 hadi 160 kwa dakika.
  • E.Iwapo sauti ya mpigo wa moyo wa fetasi ni kubwa zaidi chini ya kitovu cha mama, huenda mlalo wa fetasi hiyo ni wa kutanguliza matako.

Answer

A Sahihi. Kusikiza mpigo wa moyo wa fetasi kwa stethoskopu huitwa oskalitesheni.

B Sahihi. Kichwa cha fetasi kikiwa upande wa chini na matako ya fetasi hiyo yawe upande wa juu kwenye fandasi, huitwa mlalo wima.

C Si sahihi.Katika mlalo wa kutanguliza veteksi kitangulizi ni kichwa cha mtoto.

D Sahihi. Kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi huwa takriban mipigo 120 hadi 160 kwa dakika.

E Si sahihi. Katika mlalo wa kutanguliza matako, sauti ya mpigo wa moyo wa fetasi ni mkubwa zaidi juu ya kitovu cha mama.

Mwisho wa jibu

Soma kwa makini uchunguzi maalum ufuatao kisha ujibu maswali ya kujitathmini 11.2 hadi 11.4.

Uchunguzi maalum 11.1 Bekelech

Bekelech alikuja kwa uchunguzi katika ujauzito akiwa na ujauzito wa miezi minane. Ulipotomasa fumbatio lake, ulipata umbo gumu la mviringo kwenye fandasi ya uterasi na umbo laini kubwa karibu na kinena simfisisi. Bekelech alikuambia kuwa kucheza kwa mtoto kulikuwa kumepungua katika juma lililopita na uliposikiza kwenye fumbatio lake kwa fetoskopu hukusikia mpigo wa moyo wa fetasi.

Swali la Kujitathmini 11.2 (linatathmini Lengo la Somo 11.2)

  • a.Je, mtoto amelala wima au kingamo katika kisa cha Belekech? Eleza jinsi ulivyofikia uamuzi wako.
  • b.Je, ni nini kitangulizi katika utafiti huu?
  • c.Je, unaitaje utangulizi kama huu wa fetasi ?

Answer

  • a.Umbo gumu la mviringo kwenye fandasi ya uterasi unaweza kuwa mgongo wa mtoto na umbo kubwa laini karibu na kinena simfisisi ni mikono na miguu yake. Huu ni mlalo wima.
  • b.Matako ndiyo kitangulizi.
  • c.Huu huitwa mlalo wa kutanguliza matako.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 11.3 (linatathmini Lengo la Somo 11.3)

Je, ni wapi utakaposikiza mpigo wa moyo wa fetasi kuthibitisha utambuzi wako wa jinsi mtoto wa Bekelech alivyojilaza, na kwa nini?

Answer

Utasikiza mpigo wa moyo wa fetasi juu ya kitovu cha Bekelech kwa sababu iwapo mtoto ametanguliza matako, sauti ya mpigo wa moyo wake itakuwa kubwa zaidi hapo. (Tazama tena Mchoro 11.12 ikiwa huna uhakika.)

Mwisho wa jibu

Swali la kujitathmini 11.4 (linatathmini Malengo ya Somo 11.3na 11.4)

Je, unadhani mtoto wa Bekelech yuko katika hali gani, na ni hatua ipi unayopaswa kuchukua?

Answer

Huenda mtoto huyo ni mgojwa au hata amefariki, kwa sababu Bekelech anasema hachezi na huwezi kusikia mpigo wa moyo wa fetasi. Unapaswa kumpa rufaa aende katika kituo cha afya mara moja.

Mwisho wa jibu

Muhtasari wa Kipindi cha 11