11.1 Kujua mkao wa mtoto kwenye uterasi

Mkao wa mtoto kwenye uterasi huitwa mlalo wa fetasi. Lengo la kujua mlalo wa fetasi ni kutambua iwapo kuna dalili zozote za hatari zinazoweza kuleta ugumu katika leba na kuzaa, na kumweka mama na mtoto hatarini.

Dalili bora

  • Kuna mtoto mmoja tu kwenye uterasi.
  • Kichwa cha mtoto kiko upande wa chini wakati wa kuzaa.

Dalili za hatari

  • Mtoto ametanguliza miguu au matako wakati wa kuzaa.
  • Mtoto amelala kingamo wakati wa kuzaa.
  • Mama ana pacha wawili au watatu. Tayari unajua jinsi ya kusikiza mipigo miwili ya mioyo ya fetasi (Kipindi cha 10).

Kuna mbinu mbili za kujua mkao wa mtoto - kuhisi fumbatio la mama (utomasaji), na kusikiza (oskalitesheni) ambapo sauti ya mpigo wa moyo wa fetasi ni kubwa. Unaweza kuhitaji kutumia mbinu zote mbili ili kuwa na uhakika wa mkao wa mtoto.

Malengo ya Somo la Kipindi cha 11

11.2 Kuhisi fumbatio la mama