11.2 Kuhisi fumbatio la mama
Inaweza kuwa vigumu kujua mkao wa mtoto kabla ya miezi sita au saba ya ujauzito, na si muhimu hadi majuma 36 (miezi minane) kwa sababu ni kawaida mtoto kuzunguka hadi mwezi wa mwisho. Mara tu ujauzito unapotimiza miezi sita au saba, itakuwa rahisi kuhisi mtoto na kujua mkao wake kwenye uterasi.
Kwanza, msaidie mama kulala chali na umwekee viegemeo chini ya magoti na kichwa chake. Hakikisha ametulia. Maswali unayojaribu kujibu unapomchunguza ni:
- Je, mtoto yuko wima (juu na chini)? Huu huitwa mlalo wima.
- Au je, amelala kingamo kutoka upande mmoja hadi mwingine wa fumbatio lake? Huu ni mlalo wa kingamo.
- Je, mtoto ameangalia upande wa mbele au wa nyuma wa mama?
- Je, kichwa cha mtoto kiko chini (mlalo wakutanguliza kichwa) au matako yako chini (mlalo wakutanguliza matako)?
11.1 Kujua mkao wa mtoto kwenye uterasi