11.2.1 Je mtoto yuko wima ?

Watoto wengi huwa wamelala wima kufikia mwezi wa saba, kichwa kikiwa kimeelekea kwenye seviksi ya uterasi. Huu ndio mkao salama kabisa kwa uzazi wa kawaida. Ili kujua iwapo mtoto yuko wima, weka mkono bapa kwa kila upande wa fumbatio la mama. Finya kwa upole lakini kwa uthabiti, kwanza kwa mkono mmoja na kisha huo mwingine (Mchoro 11.1a). Chunguza umbo kwa makini. Je, miisho ya mtoto inaonekana kuwa kwenye pande za mama (Mchoro 11.1b)? Ikiwa ni hivyo, mtoto anaweza kuwa amelala kingamo. Watoto wengi hulala kingamo katika miezi ya kwanza lakini wengi hujigeuza kichwa chini kufikia miezi minane au zaidi. Watoto hawawezi kuzaliwa kupitia ukeni wakiwa katika mlalo wa kingamo. Mtoto aliyelala kingamo, na hawezi kugeuzwa leba inapoanza lazima azaliwe kwa upasuaji wa kuzaa hospitalini.

Mtoto akilala kingamo baada ya miezi minane ya ujauzito, mpe mwanamke huyo rufaa aende katika kituo cha afya.

Mchoro11.1 (a) Hisi fumbatio la mama kwa mikono yako kwa kila upande, ukisukuma pole pole kwa kila mkono kwa zamu. Unapaswa uweze kuhisi mtoto akiwa amelala wima - yaani kichwa chini. (b) Iwapo mtoto amelala kingamo, unaweza kuhisi kichwa na matako yake kwenye pande za mama.

Inaweza kuwa vigumu kuhisi mkao wa mtoto kwenye uterasi iwapo mama ana misuli yenye nguvu sana au iwapo ana mafuta mengi kwenye fumbatio lake. Iwapo itakuwa vigumu kuhisi nafasi ya mtoto mwambie mama avute pumzi nzito kisha aachilie polepole na alegeze mwili wake huku ukitomasa fumbatio lake.

11.2 Kuhisi fumbatio la mama

11.2.2 Je, mtoto ameangalia upande wa mbele au wa nyuma wa mama?