11.2.2 Je, mtoto ameangalia upande wa mbele au wa nyuma wa mama?

Kisha hisi fumbatio la mama kupata umbo kubwa gumu (mgongo wa mtoto). Iwapo utalihisi (Mchoro 11.2a), mtoto ameangalia upande wa mgongo wa mama. Iwapo huwezi kuhisi mgongo wa mtoto, tafuta vibonge vingi vidogo (Mchoro 11.2b). Iwapo unahisi vibonge vingi vidogo badala ya umbo kubwa gumu, huenda unahisi mikono na miguu ya mtoto, inayokuonyesha kuwa mtoto ameangalia upande wa mbele wa mama.

Mchoro 11.2 (a) Iwapo unahisi umbo kubwa gumu, mtoto ameangalia upande wa mgongo wa mama. (b) Iwapo unahisi vibonge vingi vidogo, mtoto ameangalia upande wa mbele wa mama.

11.2.1 Je mtoto yuko wima ?

11.2.3 Je, mtoto yuko katika hali ya kichwa chini au matako chini?