11.2.3 Je, mtoto yuko katika hali ya kichwa chini au matako chini?

Mchoro 11.3 (a) Mlalo wa kutanguliza kichwa. (b) Mlalo wa kutanguliza matako.

Kufikia mwezi wa mwisho kabla ya kuzaliwa, watoto wengi huwa wamelala kichwa kikielekea kwenye seviksi ya uterasi (Mchoro 11.3a). Hali ya kichwa chini huitwa mlalo wa kutanguliza kichwa, na iwapo sehemu ya fuvu la kichwa iitwayo veteksi itatangulia kwenye njia ya uzazi, huu ndio mlalo bora zaidi kwa uzazi wa mtoto. Madaktari na wakunga huiita sehemu ya mtoto inayotangulia kwenye seviksi ya uterasikitangulizi. Katika Mchoro 11.3a, kitangulizi ni kichwa cha mtoto na katika Mchoro 11.3b, kitangulizi ni matako ya mtoto. Utajifunza kuhusu milalo mingine (uso, paji la uso, bega) katika Moduli kuhusu Utunzaji katika Leba na kuzaa.

  • Je, veteksi ni sehemu ipi ya fuvu la kichwa? (Kumbuka Kipindi cha 6. Unaweza kutaka kutazama tena Mchoro 6.5 unaoonyesha mifupa ya fuvu la kichwa cha fetasi).

  • Veteksi ndiyo sehemu ya fuvu la kichwa cha fetasi kati ya utosi wa mbele (nafasi kati ya mifupa kwenye sehemu ya mbele ya kichwa cha mtoto), na utosi wa nyuma (nafasi kati ya mifupa kwenye sehemu ya nyuma ya kichwa cha mtoto).

    Mwisho wa jibu

11.2.2 Je, mtoto ameangalia upande wa mbele au wa nyuma wa mama?

11.2.4 Kuhisi kichwa cha mtoto