11.2.4 Kuhisi kichwa cha mtoto

Mchoro 11.4 Kutafuta mfupa wa kinena wa mama kwa vidole vyako.

Kufikia mwezi wa saba au wa nane, kichwa cha mtoto kimeteremka chini kwenye pelvisi ya mama. Hii ndiyo jinsi ya kuhisi kichwa cha mtoto:

 1. Tafuta mfupa wa kinena wa mama kwa vidole vyako. Unaweza kuuhisi chini ya ngozi iliyo chini ya vuzi za mama (Mchoro 11.4).
 2. Anapopumua nje, finya ndani juu ya mfupa wa kinena (tazama Mchoro 11.5). Finya kwa upole na uachilie iwapo unamwumiza. Ukihisi umbo gumu la mviringo unaloweza kusongesha kidogo kutoka upande mmoja hadi mwingine, huenda ni mgongo au upande wa kichwa cha mtoto.

Usipohisi chochote kwenye upande wa chini wa fumbatio la mama, huenda mtoto amelala kingamo.

Mchoro 11.5 Finya kwa uthabiti kwa vidole vyako juu ya mfupa wa kinena ujue ikiwa unaweza kuhisi kichwa cha mtoto.
 1. Ikiwa umbo hilo si la mviringo hasa, huenda ni uso au matako ya mtoto. Au wakati mwingine matako ya mtoto yako juu lakini kichwa si wima kwenda chini (Mchoro 11.6 na b) Huenda kichwa kimejikunja kuelekea upande, au kidevu kiko juu (Mchoro 11.6c). Hizi zinaweza kuwa ishara kuwa mtoto hatatoshea kupita kwenye pelvisi ya mama akizaliwa.
Mchoro 11.6 Ikiwa mtoto amelala wima na kichwa kiko chini lakini huwezi kuhisi kichwa cha mtoto, huenda kimejikunja kuelekea upande (a) kikiwa kimeangalia upande wa nyuma wa mama, (b) kimeangalia upande wa mbele wa mama, au (c) kidevu kikiwa juu.
 1. Iwapo sehemu ya chini ya mtoto haijaingia sana kwenye pelvisi ya mama, jaribu kusongesha sehemu hiyo kutoka upande mmoja hadi mwingine kwa kuitikisa polepole kwa mikono yako kila upande wa sehemu ya chini ya fumbatio lake. (Mchoro 11.7). Iwapo kusongesha sehemu ya chini ya mtoto kunaufanya mgongo wote kusonga, huenda mtoto ametanguliza matako. Ikiwa mgongo hausongi, huenda mtoto ametanguliza kichwa.
Mchoro 11.7 Ikiwa mgongo wa mtoto hausongi unapotomasa sehemu ya chini ya fumbatio, huenda kichwa cha mtoto kiko upande wa chini.
 1. Kisha hisi sehemu ya juu ya uterasi ya mama (fandasi), chini ya mbavu zake. Je, inahisi kuwa ngumu na ya mviringo, kama kichwa? Au ni umbo tofauti - kama matako, mgongo, au miguu? Ikiwa sehemu ya juu ya uterasi inahisi kama kichwa kuliko ulivyohisi kwenye sehemu ya chini ya fumbatio la mama, huenda mtoto ametanguliza matako.
 2. Weka mkono mmoja kwa mgongo wa mtoto. Wakati huo huo, kwa mkono wako mwingine, sukuma upande mwisho wa sehemu ya juu ya mtoto polepole (Mchoro 11.8). Ikiwa mgongo wote wa mtoto unasonga unaposongesha mwisho wa sehemu ya juu, huenda mtoto ametanguliza kichwa (Mchoro 11.8a). Ikiwa mgongo utabakia pale ulipo unaposongesha sehemu ya juu ya mtoto (Mchoro 11.8b), huenda unasongesha kichwa. Hii ni kwa sababu shingo linaweza kujikunja huku mgongo ukibakia mahali pake. Iwapo unasongesha kichwa kwenye sehemu ya juu ya uterasi, huenda mtoto ametanguliza matako.
Mchoro 11.8 (a) Ikiwa mtoto ametanguliza kichwa, unapaswa uweze kusongesha mgongo wake wote kwa kusukuma polepole sehemu ya juu ya mtoto upande. (b) Iwapo unaweza kusukuma sehemu ya juu ya mtoto bila kusongesha mgongo wake, huenda ametanguliza matako.
 1. Unapochunguza mkao wa mtoto, unaweza kufikiri kuwa umehisi vichwa viwili au matako mawili. Huenda mama huyo ana pacha.
 • Kumbuka Kipindi cha 10. Je, unapaswa kufanya nini ukishuku kuwa mwanamke ana pacha?

 • Mpe mama huyo rufaa aende katika kituo cha afya mara moja.

  Mwisho wa jibu

11.2.3 Je, mtoto yuko katika hali ya kichwa chini au matako chini?

11.2.5 Kumwuliza mama kuhusu kucheza kwa mtoto