11.2.5 Kumwuliza mama kuhusu kucheza kwa mtoto

Madaktari na wakunga huchukulia kucheza kwa fetasi kama ishara ya hali njema ya fetasi na pia inaweza kuashiria mlalo wa fetasi.

Huku ukihisi fumbatio la mama, jaribu kuwazia milalo tofauti ya mtoto kwenye uterasi. Wazia sehemu ambapo huenda mikono na miguu ya mtoto ipo. Wazia jinsi kila mlalo unavyoweza kumuathiri mama mtoto anapocheza. Kisha mwulize mama anakohisi mtoto akicheza kwa nguvu sana na anapohisi akicheza polepole. Je, hii ndiyo sehemu unayodhani miguu na mikono inaweza kuwa (tazama Mchoro 11.9)?

Mchoro 11.9 Sehemu ambapo mama anahisi mtoto akicheza kwa nguvu zaidi inaweza kukuonyesha ilipo miguu ya mtoto.

Mpe mwanamke rufaa aende katika kituo cha afya ikiwa hahisi mtoto akicheza ndani yake.

Mtoto akiwa na afya na anapata virutubishi vya kutosha kutoka kwa mama, yeye hucheza katika uterasi kwa njia ambayo mwanamke atamhisi. Kucheza kwa mtoto mara nyingi huhisika vizuri baada ya mama kula na baada ya kupumzika vizuri sana na amelala kwa upande.

Mwanamke akikuambia kuwa mtoto hasongi kama hapo awali, au hasongi kabisa, anaweza kuwa mgonjwa au amefariki.

11.2.4 Kuhisi kichwa cha mtoto

11.3 Kusikiza mpigo wa moyo wa mtoto