11.3.1 Kujua mkao wa mtoto kwenye uterasi kwa kusikiza mpigo wa moyo

Wazia upande ambao huenda mtoto amelalia. Kisha uanze kusikiza mpigo wa moyo karibu na sehemu unapofikiria moyo wa mtoto unapaswa kuwa. Unaweza kuhitaji kusikiza katika sehemu nyingi kwenye fumbatio la mama kabla ya kupata sehemu ambapo sauti ya mpigo wa moyo ni mkubwa na dhahiri (Mchoro 11.11).
Je, sauti ya mpigo wa moyo ni kubwa zaidi juu au chini ya kitovu cha mama? Ukisikia sauti kubwa zaidi ya mpigo wa moyo chini ya kitovu cha mama, huenda mtoto yuko katika hali ya kichwa chini (Mchoro 11.12a). Ukisikia sauti kubwa zaidi ya mpigo wa moyo juu ya kitovu cha mama, huenda mtoto yuko katika mlalo wa kutanguliza matako (Mchoro 11.12b).

Wakati mwingine, mtoto akiwa ameangalia upande wa mbele wa mama, ni vigumu kupata mpigo wa moyo kwa sababu mikono na miguu ya mtoto huzuia. Sikiza karibu na pande za mama, au moja kwa moja katikati mwa fumbatio lake ili kuusikia mpigo wa moyo wa fetasi.
11.3 Kusikiza mpigo wa moyo wa mtoto