11.4.2 Mtoto amelala kingamo

Watoto waliolala kingamo hawawezi kutoshea kwenye pelvisi ya mama ili kuzaliwa (Mchoro 11.13). Ukijaribu kuzalisha mtoto bila upasuaji, uterasi ya mama itapasuka wakati wa leba, na yeye pamoja na mtoto watafariki bila huduma ya matibabu. Mtoto akigeuka na kutanguliza kichwa wakati wowote - hata siku ambapo leba ya mama itaanza - ni SAWA kwake kuzalia nyumbani au kwenye kituo cha afya.

Mtoto aliyelala kingamo lazima azaliwe kwa upasuaji wa kuzaa hospitalini. Usijaribu kumgeuza mtoto aliyelala kingamo kwa mkono. Hii ni hatari kama kujaribu kumgeuza mtoto aliyetanguliza matako, na inapaswa kufanywa tu na daktari hospitalini.

Mchoro 11.13 Iwapo mtoto amelala kingamo kufikia mwezi wa nane, unapaswa kupanga uzazi wa hospitalini kwa upasuaji wa kuza.

11.4 Cha kufanya ukipata dalili za hatari