11.4.3 Pacha

Kumbuka uliyojifunza katika Kipindi cha 10 kuhusu ujauzito wa pacha.

  • Je, dalili tatu za ujauzito wa pacha ni zipi?

  • Uterasi hukua haraka au kubwa kuliko kawaida. Unaweza kuhisi vichwa viwili au matako mawili unapohisi tumbo la mama. Unaweza kusikia mipigo miwili ya moyo (hii si rahisi, lakini inawezekana katika miezi michache ya mwisho).

    Mwisho wa jibu

  • Je, njia mbili za kujaribu kusikia mipigo ya mioyo ya pacha ni zipi?

  • Tafuta mpigo wa moyo wa mtoto mmoja. Mwambie msaidizi kusikiza sehemu zingine ambapo mpigo wa moyo ni rahisi kusikia, na nyote mgonge mipigo ya mioyo. Tumia saa kukusaidia kuhesabu mipigo hiyo miwili ya moyo.

    Mwisho wa jibu

11.4.2 Mtoto amelala kingamo

11.5 Baada ya uchunguzi katika ujauzito