Muhtasari wa Kipindi cha 11

Katika Kipindi cha 11, umejifunza:

  1. Ni jambo la kutuliza kupata mtoto mmoja kwenye uterasi na kichwa chake kuwa upande wa chini katika mwezi wa mwisho wa ujauzito. Kufikia miezi saba ya ujauzito watoto wengi huwa wamelala wima kichwa kikielekea kwenye seviksi ya uterasi. Kufikia mwezi wa saba au wa nane, kichwa cha mtoto kwa kawaida huwa kimeteremka chini kwenye pelvisi ya mama. Huu ndio mkao salama zaidi kwa uzazi wa kawaida.
  2. Katika hali nyingine yoyote, yaani matako kuwa upande wa chini (kutanguliza matako), au amelala kingamo, mpe mama rufaa aende katika kituo cha afya kilicho karibu. Usijaribu kumgeuza mtoto aliyetanguliza matako au aliyelala kingamo.
  3. Sehemu katika fumbatio la mama anapohisi mtoto akicheza inaweza kukusaidia kutambua mkao wa mtoto huyo kwenye uterasi. Kucheza kwa fetasi pia ni ishara ya afya njema ya fetasi. Mtoto akiacha kucheza anaweza kuwa ni mgonjwa au amefariki, na mama anahitaji rufaa ya haraka.
  4. Mpigo wa moyo wa mtoto hujulisha kuhusu mkao wa mtoto kwenye uterasi ya mama na iwapo yuko hai. Kusikia mipigo miwili ya moyo ni ishara ya pacha. Sikiza mpigo wa moyo katika kila safari yake ya utunzaji katika ujauzito kuanzia miezi mitano.
  5. Kufikia miezi miwili ya mwisho ya ujauzito, unaweza kusikia mpigo wa moyo wa fetasi mara kwa mara ukiwa katika chumba kisicho na kelele kwa kuweka sikio lako kwenye fumbatio la mama. Ni rahisi kusikia mpigo wa moyo kwa stethoskopu au fetoskopu.
  6. Kiwango cha kawaida cha mpigo wa moyo wa fetasi ni takriban mipigo 120 hadi 160 kwa dakika.

Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 11