Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 12

Kwa kuwa umekamilisha kipindi hiki, unaweza kutathmini jinsi ulivyotimiza malengo ya masomo yake kwa kujibu maswali haya. Andika majibu katika shajara yako na uyajadili na Mkufunzi wako katika Mkutano Saidizi wa Masomo yatakayofuata. Unaweza kulinganisha majibu yako na Muhtasari juu ya Maswali ya Kujitathmini mwishoni mwa Moduli hii.

Swali la kujitathmini 12.1 (linatathmini malengo ya Somo 12.1 na 12.2)

Mwanamke mwenye umri wa miaka 22 aliye na ujamzito wa majuma 34 anakueleza kuwa ana tamaa ya kula udongo. Pia anakuambia kuwa amepata madoadoa ya rangi ya hudhurungi nzito usoni mwake, na kuwa nyayo na vifundo vya miguu yake huvimba mchana.

  1. Tambua matatizo madogo yanayoonekana kwa mwanamke huyu kwa kutumia majina ya kitiba.
  2. Je, utamshauri vipi ili kudhibiti dalili zake?

Answer

  1. Majina ya kitiba ya matatizo madogo ambayo mwanamke huyu anaonyesha ni kutapika, kloasma na edema.
  2. Udhibiti:

Pika: Udongo si chakula, na unaweza kumpa vimelea vinavyoweza kusababisha ugonjwa. Unastahili kumshauri asile mchanga, bali ale vyakula vyenye ayoni (kama kuku, samaki, malenge, maharagwe, mbaazi, nyama - hasa ini, figo, na nyama ya ogani zingine - na bidhaa za nafaka nzima) na vyakula vyenye kalisi (kama mboga za manjano, maziwa, magandi, mtindi, jibini, na mboga za majani ya kijani kibichi).

Kloasma: Mhakikishie kuwa madoadoa ya hudhurungi ni kawaida na yataisha baada ya mtoto kuzaliwa. Anaweza kuyapunguza kwa kuvaa kofia akiwa kwenye mwanga wa jua.

Edema: Mhimize kuweka nyayo zake juu kwa dakika chache angalau mara mbili au tatu kwa siku. Hii itasaidia kufyonza kiowevu kutoka kwenye nyayo zake hadi kwenye damu. Mhimize kula kiasi kidogo cha vyakula vilivyotayarishwa ambavyo vina chumvi nyingi na kunywa maji au juisi ya matunda kwa wingi.

Mwisho wa jibu

Swali la kujitathmini 12.2 (linatathmini Malengo ya Somo 12.1 na 12.2)

Linganisha kila tatizo na udhibiti mwafaka.

Using the following two lists, match each numbered item with the correct letter.

  1. Kula mboga na matunda kwa wingi na ukae kwenye maji baridi

  2. Kunywa chai za mitishamba zitakazomsaidia kulala

  3. Kunja wayo na kuusinga mguu kwa upole

  4. Kunywa tembe mbili za paracetamol na glasi ya maji

  5. Kuweka miguu juu na kuvaa stoki thabiti

  6. Kuvaa nguo zinazoingiza baridi, kuoga mara kwa mara na kutumia pepeo

  • a.Maumivu madogo ya kichwa

  • b.Hemoroidi

  • c.Insomnia (Ukosefu wa usingizi)

  • d.Kukakamaa miguu 

  • e.Uvarikosi kwamiguu

  • f.Kutokwa na jasho sana

The correct answers are:
  • 1 = b
  • 2 = c
  • 3 = d
  • 4 = a
  • 5 = e
  • 6 = f

Muhtasari wa Kipindi cha 12