12.3.3 Kukakamaa kwa miguu
Miguu au nyayo za wanawake wengi wajawazito zinaweza kukakamaa – haya ni maumivu makali ya ghafla na kukaza kwa misuli. Kukakamaa huku hasa hutokea usiku au wanawake wanapojinyoosha na kuvuta vidole vyao vya mguu. Ili kukomesha mikakamao, kunja wayo (kuelekea juu) na kisha usugue mguu huo kwa upole ili kuusaidia utulie (usisugue kwa nguvu).
Udhibiti
Ili kuzuia kukakamaa zaidi, mwanamke hafai kukunja vidole vyake kuelekea juu (hata anapojinyosha), na anafaa kula vyakula zaidi vilivyo na kalisi na potasiamu.
Je, unaweza kuorodhesha vyakula vilivyo na kalisi?
Mboga za manjano kama vile viazi vikuu na karoti, malimau, maziwa, magandi, mtindi, jibini, mboga zenye rangi ya kijani, vyakula vya mifupa na makaka ya mayai, molasi, maharage ya soya na dagaa.
Mwisho wa jibu
12.3.2 Maumivu ya viungo