12.3.4 Maumivu ya kighafla katika sehemu ya chini ya upande wa fumbatio
Uterasi, katika nafasi yake, hushikiliwa kwa ligamenti kwa kila upande. Ligamenti ni kiungo mithili ya kamba zinazoshikanisha uterasi kwenye fumbatio la mama. Kusonga kwa ghafla kunaweza kusababisha maumivu makali kwenye ligamenti hizi wakati mwingine. Hii si hatari. Maumivu haya hukoma baada ya dakika chache. Kusugua kwa upole au kuweka kitambaa chenye joto kwenye fumbatio kunaweza kusaidia.
12.3.3 Kukakamaa kwa miguu