12.5.2 Wasiwasi na hofu
Wanawake wengi huwa na wasiwasi wakiwa wajawazito, hasa kuhusu afya ya mtoto na kuzaa. Wasiwasi wa mwanamke kuhusu matatizo mengine maishani unaweza pia kuongezeka akiwa mjamzito. Wasiwasi kama huu ni kawaida. Haumaanishi kuwa kitu kibaya kitatokea. Wanawake walio na hisia hizi wanahitaji usaidizi wa kihisia, kama vile mtu kusikiza wasiwasi wao na kuwahimiza wahisi wenye tumaini. Pia wanaweza kuhitaji usaidizi wa kutatua matatizo waliyo nayo maishani mwao, kama vile matatizo na wenzi wao, pesa, madawa au pombe, au maswala mengine.
12.5.1 Mabadiliko ya kighafla katika hisia