Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 13

Kwa kuwa sasa umekamilisha kikao hiki, jibu maswali yafuatayo ili kubaini jinsi ulivyotimiza Malengo ya Masomo ya kipindi hiki. Andika majibu yako katika shajara yako ya masomo na uyajadili na mkufunzi wako katika Mkutano Saidizi wa Somo unaofuata. Unaweza kudhibitisha majibu yako ukilinganisha na vidokezo ulivyoandika katika Maswali ya Kujitathmini yaliyo mwishoni mwa Moduli hii.

Swali la Kujitathmini 13.1 (linatathmini Malengo ya Somo la 13.1, 13.2 na 13.4)

Ni elezo lipi ambalo si kweli?? Katika kila kauli, eleza lisilo la kweli.

  • A.Utunzaji maalum katika ujauzito huwalenga wanawake wajawazito pekee.
  • B.Wanawake katika sehemu ya kimsingi huwa na ziara 4 tu katika utunzaji maalum katika ujauzito isipokuwa wakati ishara na dalili za tahadhari zitatambulika katika awamu yoyote ile.
  • C.Wanawake wajawazito hawafai kutayarisha vifaa vyovyote vya leba na kuzaa.
  • D.Ratiba ya uzalishaji katika utunzaji maalum katika ujauzito ni sawa kwa kila mwanamke, naye hujulishwa kuhusu utunzaji huu katika ziara ya nne.
  • E.Proflaksisi katika utunzaji maalum katika ujauzito hulenga kuzuia magonjwa ya zinaa, ikiwa ni pamoja na kusambaza VVU kutoka kwa mama hadi mtoto, malaria, upungufu wa kilishe, anemia na pepopunda.

Answer

A si kweli. Utunzaji maalum katika ujauzito hauwalengi wanawake wajawazito pekee (hili lilitendeka katika mtazamo wa kitamaduni). Utunzaji maalum katika ujauzito hujumuisha mwenzi wa mwanamke na hata familia yote kumtunza mama wakati wa ujauzito, kuchunguza dalili za hatari na kujiandalia kuzaa, kujitayarishia matatizo na kupandia matukio dharura.

B ni kweli. Wanawake katika sehemu ya kimsingi huwa na ziara 4 tu katika utunzaji maalum katika ujauzito, isipokuwa ishara au dalili za tahadhari zinapogunduliwa katika awamu yoyote.

C sikweli. Mwanamke mjamzito anapaswa kujitayarishia leba na kuzaa kwa kukusanya nguo safi kabisa, wembe mpya, uzi mpya ulio safi, sabuni na burashi ya kusugua, maji safi ya kuosha na kunywa, ndoo na bakuli, vifaa vya kutengenezea vinywaji na tochi.

D si kweli. Ratiba ya kuzaa katika utunzaji maalum katika ujauzito huwa ya kibinafsi kwa kila mwanamke na mwenziwe na huheshimu matakwa na hiari ya mama. Ratiba hii hujadiliwa katika ziara ya tatu na kurudiwa inapohitajika katika ziara ya nne.

E ni kweli. Proflaksisi katika utunzaji maalum katika ujauzito hulenga kukinga magonjwa ya zinaa pamoja na kusambazwa kwa VVU kutoka kwa mama hadi mtoto, malaria, upungufu wa kilishe, anemia, maambukizi katika mfumo wa mkojo na pepopunda.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini la 13.2 (linatathmini Malengo ya Somo la 13.3 na 13.5)

Tuseme kwa mfano kwamba mwanamke mjamzito aliye na umri wa miaka 27 anayeitwa Aster amekuja kukuona. Yeye anakueleza kuwa ana mimba ya kwanza na alipata hedhi ya mwisho wiki 25 zilizopita. Ni hatua gani utakazochukua katika ziara hii ya kwanza? Kwa kawaida, ziara ya pili ya Aster itakuwa lini?

Answer

Kwa vile Aster ana mimba ya wiki 25, unapaswa kufanya huduma zote za ziara ya kwanza na ya pili za utunzaji maalum katika ujauzito. Makinika katika kuchunguza historia yake ya kimatibabu na kiukunga na ufanye uchunguzi kamili wa mwili ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu, mpigo wa moyo, halijoto, pumzi, uchunguzi wa tumbo ili kupima urefu wa fandasi, sikiliza mpigo wa moyo wa fetasi, tazama kutanguliza na mkao wa fetasi na ukague matokeo ya vipimo vya mkojo. Kusudi la hatua hizi ni kutambua iwapo Aster anafaa kufuata sehemu ya kimsingi ya utunzaji. Pia mshauri kuhusu lishe, usafi na mapumziko.

Iwapo ana afya njema na mimba inaendelea kwa hali ya kawaida, mweleze kuwa ziara itakayofuata ni kati ya wiki ya 30- 32 ya ujauzito, lakini ni sharti atafute usaidizi mara moja iwapo atapata dalili zozote za hatari, kama vile kuvuja damu, mchozo unaonuka kutoka ukeni, homa, kiwaa au kisulisuli na kuchanganyikiwa.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini la 13.3 (linatathmini Malengo ya Somo ya 13.3 na 13.5)

Tuseme Aster amekuja kwako akiwa na mimba ya wiki 32. Unatambua kuwa shinikizo lake la damu ni mmHg 120/60, ana konjaktiva iliyokwajuka kidogo na urefu wa fandasi ni wa kipimo cha fandasi ya wiki ya 38. Ishara hizi zinaonyesha nini na ni hatua zipi utakazochukua?

Answer

Konjaktiva iliyokwajuka inaonyesha kuwa huenda Aster ana anemia, hivyo mwulize kuhusu lishe yake- anakula nini na ni kiwango kipi cha chakula anachopata kila siku? Chukua vipimo vingi vya mkojo kwa kutumia kijiti cha kupimia ili kujua iwapo mkojo una sukari zaidi au protini. Ikiwa kipimo cha mkojo ni cha kawaida, mshauri kuboresha lishe na umpe tembe za foleti na ayoni.

Kwa vile fandasi ina urefu uliopita matarajio ya kawaida katika wiki ya 32 ya ujauzito, inaweza kuashiria kuwepo kwa pacha au hali ya kipatholojia na Aster anapaswa kupewa rufaa ili achunguzwe katika kiwango cha juu zaidi. Hivyo basi, unapaswa kuandika arifa ya rufaa na umshauri kuenda katika kituo cha afya au hospitali iliyo karibu. Aster anaweza kuhitaji usaidizi katika kupangia usafiri au fedha za kusafiri. Mshauri Aster kuhusu kujiandalia kuzaa, kujitayarshia matatizo na kupangia matukio ya dharura.

Mwisho wa jibu

Muhtasari wa Kipindi cha 13