13.1.1 Manufaa ya utunzaji maalum katika ujauzito

Utunzaji maalum katika ujauzito umepata umaarufu kwa sababu ya manufaa yake katika kupunguza vifo vya kina mama na uwezo wa kufa na maradhi(ugonjwa, matatizo au ulemavu) ya kipindi kinachokaribiana na kuzaliwa. Uwezo wa kufa katika kipindi kinachokaribiana na kuzaliwa ni idadi ya jumla ya uzazimfu (watoto wanaozaliwa wafu baada ya wiki 28 za ujauzito) ikijumlishwa na idadi ya jumla ya watoto wachanga (watoto wazawa) ambao hufariki katika siku 7 za kwanza za maisha. Kima cha vifo katika kipindi kinachokaribiana na kuzaliwa ni idadi ya watoto wanaozaliwa wafu na vifo vya watoto wachanga vinavyotokea kwa kila watoto 1000 waliozaliwa hai, na ni kipimo kilichotambulika ulimwenguni kote cha kiwango cha utunzaji katika ujauzito.

  • Ufasili wa uwiano wa kiwango cha vifo vya kina mama ni upi? (Ulijifunza haya katika Kipindi cha 1 cha Moduli hii.)

  • Uwiano wa kiwango cha vifo vya kina mama ni idadi ya jumla ya wanawake wanaofariki kutokana na matatizo ya ujauzito au kuzaa, kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa hai.

    Mwisho wa jibu

Utunzaji katika maalum ujauzito ni mtazamo mwafaka kwa nchi zisizo na raslimali za kutosha ambapo wataalamu wa afya ni wachache na miundo msingi ya afya ni duni. Hususani, wanawake wengi wajawazito hawawezi kukimu gharama ya ziara za kila mara kama inavyohitajika katika mtazamo wa kitamaduni wa utunzaji katika ujauzito. Katika mtazamo wa kimipango na kifedha, mtazamo wa kitamaduni wa utunzaji katika ujauzito hauwezi kutekelezwa katika wanawake wengi wajawazito na ni mzigo kwa mfumo wa afya. Kwa hivyo, mataifa mengi yanayoendelea yanachukua mtazamo wa utunzaji maalum katika ujauzito.

13.1 Dhana na kanuni za utunzaji maalum katika ujauzito

13.1.2 Kasoro za mtazamo wa kitamaduni wa utunzaji katika ujauzito