13.1.2 Kasoro za mtazamo wa kitamaduni wa utunzaji katika ujauzito

Utafiti (kwa mfano, tazama Kisanduku13.2) umeonyesha kuwa ziara za kila mara za kipindi cha ujauzito kama ilivyo katika mtazamo wa kitamaduni haziboreshi matokeo ya ujauzito. Hususan, wanawake wajawazito unaoitajika kuwa na 'hatari ya chini' au 'wasio na hatari' katika mtazamo wa kitamaduni wa utunzaji katika ujauzito huenda wasipate ushauri kuhusu dalili za hatari. Hivyo, mara nyingi wanawake hawa hawatambui dalili za hatari hivyo hawawaarifu wataalamu wa afya haraka iwezekanavyo.

Kisanduku 13.2 Kukosa kutambua mimba 'zilizo hatarini'

Kwa kuchukua kutokea kwa leba iliyokwama kama mojawapo ya kiashiria, utafiti wa mwaka wa 1984 nchini Zaire katika wanawake 3,614 wajawazito ulionyesha kuwa asilimia 71 ya wanawake walio na leba iliyokwama walikuwa wameainishwa kama 'wasio na hatari' hapo awali, wakati asilimia 90 ya wanawake waliogunduliwa kuwa 'katika hatari' hawakupata leba iliyokwama. Hii ni asili moja ya ushahidi kuonyesha kuwa matatizo mengi ya ujauzito hayawezi kutabirika na hutokea katika awamu za mwisho.

Mifano mingine ya matatizo ya ujauzito yasiyoweza kutabirika ambayo hutokea katika awamu za mwisho zaidi za ujauzito hujumuisha visababishi vitatu vikuu vya vifo vingi vya kina mama:

  • Matatizo ya hipatensheni katika ujauzito (hipatensheni humaanisha shinikizo la juu la damu hasa eklampsia, ambayo kwa kawaida hutokea katika ujauzito awamu za mwisho za ujauzito, wakati wa leba au baada ya kuzaa (utajifunza haya katika Kipindi cha 19).
  • Kuvuja damu (kuvuja damu nyingi) kwa kawaida hutokea katika trimesta ya tatu (Kipindi cha 21 kinaeleza kuvuja damu katika awamu za mwisho za ujauzito) au hasa hali hatari ya kuvuja damu baada ya kuzaa, ambayo hutokea baada ya kuzaa (utajifunza haya katika Moduli ya Utunzaji wa Leba na Kuzaa).
  • Maambukizi yanayohusiana na ujauzito (Maambukizi ya uterasi baada ya kuzaa) ambayo kwa kawaida hutokea baada ya kuzaa (kama ilivyoelezwa katika Moduli ya Utunzaji wa Leba na Kuzaa).

Mtazamo wa kitamaduni wa utunzaji katika ujauzito umeshindwa kutambua kwa hakika wanawake walio ’katika hatari' ya kupata hali hizi zinazotishia maisha. Mtazamo huu hutambua baadhi ya wanawake kama walio na 'hatari ya chini' ambao baadaye hupata dalili za hatari zinazohitaji wataalamu kuingilia kati kwa dharura.

13.1.1 Manufaa ya utunzaji maalum katika ujauzito

13.1.3 Ulinganishaji wa utunzaji katika ujauzito wa kitamaduni na utunzaji maalum