13.2 Vipengele muhimu vya utunzaji maalum katika ujauzito

Utunzaji maalum katika ujauzito una awamu tatu zifuatazo:

  • Uchunguzi kamili (kuchukua historia, uchunguzi wa kimwili na upelelezi wa kimsingi)
  • Kuingilia kati (kuzuia/ proflasksisi na matibabu)
  • Uhamasisho (elimu ya afya/ kushauri na kusambaza utunzaji wa afya).

Kisanduku 13.3 kinatoa muhtasari wa hatua za utaratibu huu.

Kisanduku 13.3 Hatua za kimsingi katika huduma ya utunzaji maalum katika ujauzito

  1. Kusanya habari (chukua historia) kwa kuzungumza na mama, kuchunguza mwili wake na wa fetasi (uchunguzi wa mwili na vipimo), kama ulivyojifunza katika Vipindi vya 8-11 vya Moduli hii.
  2. Tafsiri habari uliyokusanya (fanya utambuzi) na utathmini vipengele vyovyote vilivyo vya hatari.
  3. Tengeneza ratiba ya utunzaji wa kibinafsi. Ratiba ya utunzaji italenga ushauri, maandalizi ya kuzaa na kiwango cha kujitayarishia matatizo ikiwa hakuna matatizo yatakayotambuliwa. Ikiwa mama anahitaji utunzaji maalum, ratiba hii itakuwa ya kumpa mama rufaa hadi kwenye kituo cha afya cha juu zaidi.
  4. Fuata ratiba ya utunzaji - katika ziara zinazofuatia, unaweza kumhudumia mwanamke wewe binafsi kwa kutoa matibabu na ushauri au pengine utahitaji kumpa rufaa.

Katika utoaji huduma ya utunzaji maalum katika ujauzito vipengele muhimu vitakavyozingatiwa ni:

  • Kuweka siri na faragha; mawasiliano mwafaka hujenga uaminifu na kukuza ujasiri, hivyo unapaswa kuzungumza na mwanamke na mumewe kwa njia inayochochea mawasiliano kuhusu maandalizi ya kuzaa, kujitayarishia matatizo, kuzuia VVU, utunzaji na matibabu.
  • Utunzaji endelevu hutolewa na mhudumu yule yule kwa wanawake wajawazito katika jamii; katika muktadha wa mtalaa huu, wewe ndiwe mtaalamu wa kutoa huduma ya utunzaji kwa wanawake wajawazito wasio na matatizo yaliyotambulika.
  • Kuhamasisha uhusika wa mwenzi wa mwanamke au msaidizi katika shughuli ya utunzaji katika ujauzito na matayarisho ya kuzalisha.
  • Kutoa huduma ya kidesturi ya utunzaji katika ujauzito kama ilivyo katika itifaki za kitaifa, kama itakavyoelezwa baadaye katika kipindi hiki).
  • Kuunganisha utunzaji katika ujauzito na wa baada ya kuzaa pamoja na kuzuia kusambazwa kwa VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto na kutoa huduma za upangaji uzazi.

13.1.3 Ulinganishaji wa utunzaji katika ujauzito wa kitamaduni na utunzaji maalum

13.3 Vipengele vya kimsingi na maalum vya utunzaji maalum katika ujauzito