13.3 Vipengele vya kimsingi na maalum vya utunzaji maalum katika ujauzito

Kielelezo cha utunzaji maalum katika ujauzito huwaainisha wanawake wajawazito katika vikundi viwili: wanaostahiki kupata utunzaji wa kidesturi katika ujauzito (kikundi kinachoitwa kipengele chakimsingi), na wanaohitaji utunzaji maalum kulingana na hali yao hasa ya afya au vipengele vya hatari (kipengele maalum). Vigezo vilivyowekwa awali (kama inavyoelezwa hapa chini) hutumika kuamua kuhusu wanawake wanaostahiki kuingia katika kipengele cha kimsingi. Wanawake waliochaguliwa kuwa katika kipengele cha kimsingi huchukuliwa kama wasiohitaji ukaguzi zaidi au utunzaji maalum wakati wa ziara ya kwanza, bila kuzingatia umri wa ujauzito ambao mama alianza ratiba ya utunzaji katika ujauzito.

Wanawake huulizwa maswali na kuchunguzwa katika ziara ya kwanza ili kufahamu iwapo wana vipengele vyovyote vifuatavyo vya hatari:

Mimba ya awali:

  • Ilitokea kuwa uzazimfu au kifo cha mtoto mzawa
  • Historia ya utokaji wa ghafla wa mara tatu au zaidi mfululizo
  • Mtoto mwenye uzito wa chini (4000 g) wakati wa kuzaliwa
  • Kulazwa hospitalini kufuatia shinikizo la juu la damu, prieklampsia au eklampsia. (Utajifunza kuhusu hali hizi katika Kipindi cha 19.)

Mimba iliyopo:

  • Utambuzi au kukisia kuwepo kwa mimba ya pacha au watoto wengi
  • Umri wa mama ukiwa chini ya miaka 16 au zaidi ya 40
  • Mama ana aina ya damu isiyo na antijeni ya Rhesus:hali hii inaweza kusababisha madhara makubwa kwa fetasi ikiwa damu ya fetasi ina antijeni ya Rhesus, kwa sababu mwili wa mama hutolesha antibodi zinazoweza kupitia kwenye plasenta na kuvamia tishu za mtoto
  • Mama anavuja damu ukeni au ana uvimbe katika pelvisi
  • Shinikizo la damu ya mama la kidiastoli (kiwango cha chini) ni mmHg 90 au zaidi
  • Kwa sasa mama ana kisukari, ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa figo, saratani, shinikizo la juu la damu au maradhi yoyote makali ya kuambukiza kama vile tibii, malaria, VVU/UKIMWI au magonjwa mengine ya zinaa.

'NDIO' kwa MOJAWAPO ya maswali yaliyoko hapo juu humaanisha kuwa mwanamke huyo hastahiki kuwa katika kipengele cha kimsingi ya utunzaji katika ujauzito. Mwanamke huyu ataainishwa katika kipengele maalum na anahitaji kuangaliwa kwa makini zaidi na kupewa rufaa kwa utunzaji wa kitaalamu.

Utawapa rufaa wanawake walio katika kipengele maalum ili wafuatiliwe kwa makini zaidi katika kituo cha afya cha kiwango cha juu zaidi na kupewa utunzaji maalum utakaoamuliwa na wataalamu katika nyenzo hizo, hali ukiendelea kufuata hatua zilizoko katika kipengele cha kimsingi.

13.2 Vipengele muhimu vya utunzaji maalum katika ujauzito

13.4 Kadi ya utunzaji katika ujauzito