13.5.2 Ziara ya pili ya utunzaji maalum katika ujauzito
Ratibu ziara ya pili ya utunzaji maalum katika ujauzito kati ya wiki ya 24-28 ya ujauzito. Fuata taratibu zilizoelezwa katika ziara ya kwanza. Aidha:
- Zingatia malalamishi au mashaka yoyote ya mwanamke mjamzito na ya mwenziye.
- Kwa wale wanaozaa kwa mara ya kwanza au yeyote aliye na historia ya shinikizo la juu la damu au prieklampsia/eklampsia, pima kiwango cha protini katika mkojo wake kwa kutumia kijiti cha kupimia. (Utajifunza jinsi ya kufanya hivi katika Kipindi cha 19 cha Moduli hii.)
- Durusu, na iwapo itahitajika, ubadilishe ratiba yake ya utunzaji wa kibinafsi.
- Mpe ushauri kuhusu mahali popote anapoweza kupokea usaidizi wa kijamii au kifedha unaoweza kupatikana katika jamii yake.
Back to previous pagePrevious
13.5.1 Ziara ya kwanza ya utunzaji maalum katika ujauzito