13.5.3 Ziara ya tatu ya utunzaji maalum katika ujauzito

Ziara ya tatu ya utunzaji maalum katika ujauzito inapaswa kutendeka karibu na kipindi cha wiki ya 30- 32 ya ujauzito. Malengo ya ziara hii ya tatu ni sawa na yale ya ziara ya pili. Aidha: unapaswa:

  • Kumakinika zaidi kuhusu ishara za mimba ya watoto wengi na umpe rufaa ukikisia kuwepo kwa zaidi ya fetasi moja.
  • Kudurusu ratiba ya kujiandalia kuzaa na ile ya kujitayarishia matatizo (iliyojadiliwa baadaye katika kipindi hiki)
  • Kupima kiwango cha protini katika mkojo wa wanawake wote wajawazito kwa kutumia kijiti cha kupimia (kwani matatizo ya shinikizo la juu la damu hayatabiriki pamoja na matukio ya awamu za mwisho za ujauzito)
  • Kuamua iwapo kuna haja ya rufaa kulingana na ugaguzi wa hivi karibuni wa hatari.
  • Kumshauri kuhusu upangaji uzazi (Kipindi cha 14).
  • Kumhimiza mama azingatie kunyonyesha mtoto bila kumpa chakula kingine chochote (Kipindi cha 14).

Kumbuka kuwa wanawake wengine huenda wakapata leba kabla ya ziara inayofuata. Washauri wanawake wote kukuita mara moja au kuja kwako punde tu wanapoanza leba. Usingoje!

Unapaswa pia kusisitiza umuhimu wa ziara ya kwanza baada ya kuzaa ili kuhakikisha umemhudumia akiwa nyumbani kwake au kituoni cha afya baada ya kuzaa. Kipindi kilicho muhimu zaidi baada ya kuzaa ni saa 4 za kwanza; matukio mengi ya kuvuja damu baada ya kuzaa hutokea wakati huu. (Utajifunza kuhusu kuvuja damu baada ya kuzaa katika Moduli ya Utunzaji katika Leba na Kuzaa.)

13.5.2 Ziara ya pili ya utunzaji maalum katika ujauzito

13.5.4 Ziara ya nne ya utunzaji maalum katika ujauzito