13.5.4 Ziara ya nne ya utunzaji maalum katika ujauzito

Ziara ya nne ya utunzaji maalum katika ujauzito inapaswa kuwa ya mwisho kwa wanawake walio katika kipengele cha kimsingi na hupaswa kufanyika kati ya wiki ya 36- 40 ya ujauzito. Unapaswa kuzingatia hatua zote zilizoelezwa katika ziara ya tatu. Aidha:

  • Uchunguzi wa tumbo unapaswa kutambua jinsi fetasi imejilaza na sehemu itakayotangulia katika uterasi, kama ulivyojifunza katika Kipindi cha 10 na 11 na katika masomo ya kiutendaji. Katika ziara hii, ni muhimu kuwatambua wanawake walio na mtoto aliyetanguliza matako au mwenye mkao wa kukingama, kisha umpe rufaa hadi kwenye kituo cha afya kilicho karibu ili apate ukaguzi wa kiukunga.
  • Ratiba ya kibinafsi ya kuzaa (Kisanduku 13.4) inapaswa kudurusiwa ili kutambua iwapo inajumuisha vipengele vyote vya kujitayarishia kuzaa, kujiandalia matatizo na kupangia matukio ya dharura, kama inavyoelezwa katika kitengo kinachofuata.
  • Mpe mama ushauri kuhusu ishara za leba ya kawaida na mambo ya dharura ya nayohusiana na ujauzito (kama ilivyoelezwa katika Kipindi cha 15), jinsi ya kukabiliana na hali hizi, ikijumuisha mahali anapopaswa kutafuta usaidizi.
  • Kutanguliza matako, na mkao wa kukingama humaanisha nini? (Ulijifunza haya katika Kipindi cha 11.)

  • Kutanguliza matako ni hali ambapo kichwa cha mtoto kinaelekea juu katika uterasi, huku matako, miguu au nyayo zikielekea chini kwenye seviksi ya mama wakati ujauzito unapokaribia mwisho. Mkao wa kukingama ni hali ambayo mtoto amejilaza kutoka upande mmoja hadi mwingine katika fumbatio.

    Mwisho wa jibu

Mtoto aliyetanguliza matako huenda azaliwe kupitia uke katika kituo cha afya. Mtaalamu wa kiukunga anaweza kumrekebisha mtoto aliyejilaza kwa kukingama hadi arejelee hali ya kawaida ya kutanguliza kichwa au veteksi, au ni sharti azaliwe kwa upasuaji.

Kisanduku 13.4 Ratiba ya kibinafsi ya kuzaa

Ratiba ya kibinafsi ya kuzaa ni mwongozo wa wahudumu wa afya inayoanzishwa kwa kujadiliana na mwanawake binafsi na mwenzi wake au wasaidizi wakuu. Mwongozo huu huonyesha jinsi wangependa kuzaa. Baadhi ya wachumba huchagua kuzalia nyumbani chini ya utunzaji wako kwa sababu wao huchukulia kuzaa kama jambo la kawaida maishani. Wengine huchagua kuzalia hospitalini au katika kituo cha afya. Ratiba ya kuzaa ya wanawake walio na VVU inapaswa kuwa kuzalisha katika kituo cha afya kama ilivyo katika Mwelekezo wa Kitaifa wa kuzuia kusambazwa kwa VVU kutoka kwa mama hadi mtoto (kama ilivyoelezwa katika Kipindi cha 16).

13.5.3 Ziara ya tatu ya utunzaji maalum katika ujauzito

13.6 Kujitayarishia kuzaa, kujiandalia matatizo na kupangia hali za dharura