13.6.1 Kujitayarishia kuzaa kwa njia ya kawaida

Muelimishe mama na familia yake kubaini ishara za kawaida za leba. Mwanamke anaweza kuzaa siku kadhaa au hata wiki nyingi kabla au baada ya tarehe iliyotarajiwa, kulingana na tarehe ya kipindi cha mwisho cha hedhi ya kawaida. Mwanamke anapofahamu maana ya leba, ataweza kufahamu kitakachotokea. Ufahamu huu kisha humsaidia kutulia zaidi na kuwa na ujasiri katika siku au wiki za mwisho za ujauzito.

Toa maagizo dhahiri ya jambo la kufanya leba inapoanza (kwa mfano ikiwa atakuwa na maumivu ya mkakamao wa misuli ya fumbatio au kuvuja kwa kiowevu cha amniotiki). Hakikisha kuwa kuna mtu atakayekuita wewe au mtaalamu mwingine ili kuzalisha haraka iwezekanavyo. Ambatanisha ushauri wako wa kiusemi kwa maagizo yaliyoandikwa kwa lugha asili ya mteja.

Maandalizi ya kuzaa pia yanafaa kuzingatia:

  • Kuheshimu chaguo la mama. Unapaswa kumpa mama habari zote zinazohitajika kuhusu uzalishaji safi na salama, lakini hatimaye unapaswa kuheshimu chaguo lake kuhusu mahali pa kuzalia na mtu angelipenda kuandamana naye.
  • Kumsaidia mama kutambua mahali pa kupata usaidizi wakati wa kuzaa na kipindi cha baada ya kuzaa kinachofuata punde.
  • Kupangia gharama yoyote ya ziada inayohusiana na kuzaa.
  • Kutayarisha vifaa vya kumtunza mama na mtoto wake mzawa.

13.6 Kujitayarishia kuzaa, kujiandalia matatizo na kupangia hali za dharura

13.6.2 Vifaa vya kuzalishia ambavyo mama anapaswa kutayarisha