13.6.2 Vifaa vya kuzalishia ambavyo mama anapaswa kutayarisha
Vifaa vya kuzalishia ambavyo mwanamke mjamzito na familia yake wanapaswa kushauriwa watayarishe kabla ya kuzaa ni (tazama Mchoro 13.2):
- Nguo safi kabisa za mama kulalia na za kumpangusa mtoto mzawa na kumfunika
- Wembe mpya wa kukata kambakitovu
- Uzi safi mpya wa kufungia kitovu
- Sabuni, burashi ya kusugua na (ikiwezekana) alkoholi ya tiba ili kutakasa
- Maji safi ya kunywa, kumwosha mama na mikono yako.
- Ndoo tatu kubwa au bakuli.
- Vifaa vya kutengenezea vinywaji vya kuongeza maji mwilini, 'atmit’ au chai.
- Tochi ikiwa hakuna umeme katika eneo lile.
Back to previous pagePrevious
13.6.1 Kujitayarishia kuzaa kwa njia ya kawaida