13.6.3 Kujiandalia matatizo na kupangia matukio ya dharura

Kama ilivyodokezwa hapo awali, kujiandalia matatizo ni utaratibu wa kutazamia hatua zinazohitajika ikiwa jambo la dharura litatokea, na pia kufanya mpango wa dharura (Kisanduku 13.5). Matatizo yanayohusiana na ujauzito kama vile shinikizo la juu la damu na kuvuja damu yanaweza kutokea wakati wowote katika ziara za utunzaji katika ujauzito, na ugonjwa wowote unaweza kutokea wakati wa ujauzito. Hali hizi zinapokisiwa katika awamu yoyote ya ujauzito, unapaswa kumpa mwanamke huyo rufaa mara moja na urudie kumshauri aje kukuona au kutafuta huduma ya kitabibu haraka iwapo dalili za hatari zitaonekana.

Kisanduku 13.5 Katika hali ya dharura

Hakikisha kuwa mwanamke na mumewe pamoja na watu wengine katika familia wanajua mahali pa kutafuta usaidizi.

  • Waharifu kupangia usafiri kwa kuwasiliana na wamiliki gari.
  • Wahimize kuweka hakiba ya pesa za usafiri, dawa na matibabu mengine.
  • Amua ni nani ambaye ataandamana na mama hadi kwenye kituo cha afya.
  • Amua ni nani atakayeitunza familia wakati mama hayupo.
  • Mwanamke mjamzito anaweza kuvuja damu kwa wingi wakati wa kuzaa au baada ya kuzaa hivyo anaweza kuhitaji kuongezewa damu. Hakikisha kuwa mama mjamzito au mume wake amewatambua watu wazima wawili wenye afya watakaokubali kumtolea damu ikiwa mama atahitaji. Wahakikishie watu wanaopangia kutoa damu kuwa hawataathirika kwa kutoa damu, na kwamba afya yao ya kijumla itakaguliwa kabla ya kutoa damu.

Sehemu muhimu ya kupangia matukio ya dharura ni kutazamia matukio yanayoweza kusababisha kukawia kunakoweza kuepukwa kwa mipango bora.

13.6.2 Vifaa vya kuzalishia ambavyo mama anapaswa kutayarisha

13.6.4 Visababishi vya kuchelewa kupata usaidizi wa dharura