13.6.4 Visababishi vya kuchelewa kupata usaidizi wa dharura

Kuna aina tatu ya kuchelewesha usaidizi. Zote zinaweza kuwa hatari kwa mama na mtoto wake:

  • Mazoea ya kuchelewa kutafuta huduma ya kiafya (kukawia kuamua kutafuta huduma ya kimatibabu),
  • Kuchelewa kufika kwenye kituo cha afya
  • Kuchelewa kupata matibabu mwafaka.

Kuchelewa huku husababishwa na vipengele kadhaa, vikiwemo vikwazo vya kimipango na kifedha, na ukosefu wa maarifa kuhusu maswala ya kiafya ya kina mama na watoto wazawa. Kwa mfano, mama, familia yake na hata majirani wanaweza kuhisi kuwa ni mume tu au mtu mwingine wa familia aliyeheshimiwa anayeweza kumpa ruhusa mama akuite au apate huduma ya matibabu ya haraka katika kituo cha afya. Lakini kukawia huku kunaweza kuhatarisha maisha yake na ya mtoto.

Kuchelewa kuamua kutafuta huduma kunaweza kusababishwa na kushindwa kutambua dalili za matatizo, maswala kuhusu gharama, matukio mabaya ya awali kuhusu mfumo wa huduma ya afya na matatizo ya kiusafiri. Kuchelewa kufikia huduma kunaweza kusababishwa na umbali wa nyumba ya mwanamke mjamzito hadi kwenye kituo cha afya au mhudumu wa afya, hali ya barabara au ukosefu wa usafiri wa dharura.

Kuchelewa kupata huduma mwafaka kunaweza kupelekea upungufu wa vifaa vya kimsingi, ukosefu wa wataalamu wa afya na ujuzi duni wa wahudumu wa afya. Visababishi vya kukawia huku hutokea mara nyingi na vinaweza kutabirika. Hata hivyo, wanawake wajawazito, familia na jamii, wahudumu na vituo vya afya vilivyo karibu ni sharti wajitayarishe mapema kuchukua hatua za haraka iwapo dharura itatokea.

13.6.3 Kujiandalia matatizo na kupangia matukio ya dharura

13.6.5 Kufanya rufaa