13.6.5 Kufanya rufaa

Hatimaye, unapaswa kufahamu hatua ya kuchukua unapofanya rufaa - kumhamisha mgonjwa ili apate huduma zaidi ya kiafya na utunzaji maalum katika kituo cha afya cha kiwango cha juu zaidi. Unapaswa kujaza fomu ya rufaa kikamilifu na utie sahihi na tarehe, kisha uhakikishe inaambatana na mteja kwenye kituo cha afya ulichomhamishia; fomu hii pia ina nafasi ya majibu kutoka kituoni kuhusu matibabu waliyompa mgonjwa.

Ikiwa hauna fomu sanifu ya rufaa, unapaswa kuandika arifa iliyo na taarifa muhimu (Kisanduku 13.6).

Kisanduku 13.6 Arifa ya rufaa

  • Tarehe na wakati wa rufaa
  • Jina la kituo cha afya unachomtuma mteja
  • Jina, tarehe ya kuzaliwa, nambari ya kitambulisho (iwapo inajulikana) na anwani ya mteja
  • Historia muhimu ya kitabibu ya mteja
  • Matokeo ya uchunguzi wa kimwili na vipimo
  • Utambuzi unaokisiwa
  • Matibabu yoyote uliyompa mteja
  • Sababu ya kumpa mteja rufaa
  • Jina lako, tarehe na sahihi.

Hii ndiyo tamati ya mjadala wetu kuhusu utunzaji maalum katika ujauzito. Katika vipindi vinavyofuata katika Moduli hii, utajifunza zaidi kuhusu vipengele maalum vya utunzaji katika ujauzito katika maandhari mahususi, pamoja na maswala ya uhamasisho wa kiafya katika ujauzito, kumshauri mwanamke mjamzito kuhusu dalili za hatari, kuzuia kusambazwa kwa VVU kutoka kwa mama hadi mtoto, utambuzi na udhibiti wa malaria, anemia na maambukizo ya mfumo wa mkojo, shinikizo la juu la damu, huaribikaji wa mimba na kuvuja damu katika awamu za kwanza na za mwisho za ujauzito. Moduli ya Utunzaji katika ujauzito inamalizia kwa kueleza jinsi ya kuingiza kanula na neli ndani ya mishipa ya vena ili kutia viowevu moja kwa moja katika mkondo wa damu na jinsi ya kuingiza katheta ya mkojo ili kumsaidia mama mjamzito kukojoa. Vipindi vya mafunzo ya kiutendaji vitahakikisha kuwa umepata maarifa haya.

13.6.4 Visababishi vya kuchelewa kupata usaidizi wa dharura

Muhtasari wa Kipindi cha 13