Muhtasari wa Kipindi cha 13

Katika Kipindi cha 13 umejifunza kwamba:

  1. Utunzaji maalum katika ujauzito hutenganisha wanawake wajawazito wanaofaa kupata utunzaji wa kidesturi katika ujauzito (kipengele cha kimsingi) na wale wanaohitaji utunzaji maalum katika hali mahususi za kiafya au vipengele vya hatari.
  2. Utunzaji maalum katika ujauzito husisitiza kupanga utunzaji wa kibinafsi na wa watu waliolengwa na kupangia kuzaa.
  3. Utunzaji maalum katika ujauzito humfanya mwanamke mjamzito pamoja na mumewe na familia kushiriki katika utambuzi wa matatizo yanayohusiana na yasiyohusiana na ujauzito, kupangia na kufanya uamuzi kuhusu mwendo wa baadaye wa ujauzito.
  4. Hakuna mimba inayoweza kuwa 'bila hatari' hadi ithibitishwe.
  5. Mwanamke mjamzito ana ziara nne za utunzaji katika ujauzito na kila ziara ina malengo maalum ya kuhamasisha kuhusu utunzaji, afya ya mama na fetasi, kukadiria hatari na kufanya utambuzi wa mapema wa matatizo.
  6. Ziara ya kwanza ya utunzaji maalum katika ujauzito inapaswa kuwa kabla ya wiki ya 16 ya ujauzito; hukagua historia ya kimatibabu na kiukunga ya mwanamke, uchunguzi wa kimwili na matokeo ya vipimo ili kuamua iwapo mama anafaa kufuata sehemu ya kimsingi.
  7. Ziara ya pili ya utunzaji maalum katika ujauzito huwa kati ya wiki ya 24-28 ya ujauzito. Lengo zaidi ni kupima shinikizo ya damu na urefu wa fandasi ili kufahamu umri wa ujauzito.
  8. Ziara ya tatu ya utunzaji maalum katika ujauzito huwa kati ya wiki ya 30-32 ya ujauzito. Lengo la ziada ni kutambua iwapo mama amebeba mimba ya watoto wengi.
  9. Ziara ya nne ya utunzaji maalum katika ujauzito huwa ya mwisho kati ya wiki ya 36 na 40 ya ujauzito. Lengo la ziada ni kugundua ikiwa fetasi inatanguliza matako, iwapo ina mkao wa kukingama, na ishara za matatizo ya shinikizo la juu la damu. Makinika zaidi kuwaeleza wanawake kuhusu kujitayarishia kuzaa, kujiandalia matatizo na kupangia matukio ya dharura.
  10. Kujiandalia matatizo na kupangia matukio ya dharura hutazamia na kutayarishia hatua zinazohitajika iwapo jambo la dharura litatokea, ikiwa ni pamoja na kupangia usafiri, fedha, wasaidizi na watu waa kutoa damu na kupunguza mambo yanayopelekea kukawia kufika kwenye kituo cha afya cha kiwango cha juu zaidi.
  11. Wanawake wanaohitaji rufaa katika awamu yoyote ya ujauzito, au leba inapoanza wanapaswa kuandikiwa arifa ya rufaa iliyo na maelezo ya historia yao, utambuzi na matibabu.

13.6.5 Kufanya rufaa

Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 13